Burudani

Iggy Azalea: Nimeibadilisha Hip Hop

Rapper mwenye asili ya nchini Australia, Iggy Azalea, amesema anaamini hadi sasa amefanikiwa kuleta mabadiliko kadhaa kwenye muziki wa hip hop.

iggy-azalea

“Kama nikiwa na career iliyodumu kwa kipindi kifupi, walau naweza kusema nimesababisha tofauti,” anasema rapper wa Australia, Iggy Azalea kwenye mahojiano na jarida la GQ.

“Huwezi kujua ni kwa muda gani utakuwa kwenye neema za watu hususan kwenye biashara hiyo. Hivyo naamini career yangu ni ndefu – lakini naweza kuwa hapa kwa miaka mitatu au minne na kisha kuondoka, kama wasanii wengi.”

Rapper huyo anasema hana wasiwasi kuhusu kama ataweza kudumu kwenye muziki lakini anaamini ameweza kuleta mabadiliko ya kipi kinachokubalika kwenye muziki huo.
Iggy amekuwa akikabiliana na ukosoaji mwingi kwa mtindo wake wa kurap na ile kuwa rapper wa kizungu.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents