Burudani

Irene Uwoya awafungukia, ‘Nikivaa nguo za ufukweni nipo uchi mke wa mtu’

Muigizaji wa filamu Bongo, Irene Uwoya amewafungukia wale wanaokosoa vazi lake la ufukweni.

Mrembo huyo ambaye ni mke wa msanii wa Dogo Janja amesema yeye si wa kwanza kufanya hivyo. Kupitia Instagram ameandika;

Ukivaaa nguo kawaida anakigodoro, nikimpost mume ooh mdogo, nisipo post kwanini humpost humpendi. Nikivaaa nguo za ufukweni nipo uchi mke wa mtu.

Sasa nasema hivi kwa wale iliyowauma poleeeni sanaaa, siku nyingine nitawashirikisha nikitaka kuposti, hivi kaka @loydemich mimi ni wakwanza kwani bongo kuvaaa hivi maeneo ya ufukweni?: mme wangu kaipenda balaaah yaani.


Irene Uwoya na Dogo Janja waliripotiwa kufunga ndoa November 25, 2017, hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili kutokana na namna walivyoliweka suala hilo hasa kwa upande wa vyombo vya habari na mitandao kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents