Burudani

Jaguar amchana Harmonize ishu ya kushindwa kutumbuiza Eldoret ‘ni dharau, amewakosea mashabiki wake Kenya’

Msanii wa muziki nchini Kenya, Jaguar amefunguka sakata la Harmonize kushindwa kutumbuiza wikiendi iliyopita mjini Eldoret baada ya kuzinguana na Promota aliyeandaa tamasha hilo.

Image result for jaguar kenya
Jaguar

Jaguar amesema kuwa kitendo cha Harmonize kushindwa kupanda jukwaani kutumbuiza, mbele ya mashabiki wake elfu 5 waliolipia kiingilio kwenye show hiyo ni dharau, kwani alitakiwa atumbuize halafu amalizane na promota wake baadae.

Ni tukio la kuhuzunisha lakini mimi namshutumu sana Harmonize….wakenya wamem-support sana, wame-support wasanii wa nje sana. Wengine wanatumia pesa zao kupiga simu, kurequest nyimbo zao. Mimi mwenyewe siwezi nikakosa kupanda stage sababu ya balance ambayo promoter amebakisha na ni kitu nilikuwa nafanya. Kwanza nadeal na mafans wangu. Kama Mimi ningekuwa Harmonize Saturday ningeenda kwa stage niambie watu samahani nimechelewa lakini kwa sababu mumenifikisha mahali nimefika saa hii mimi nitaperform lakini promoter hajanilipa…vitu zingine nitadeal nazo baadaye sababu bila nyinyi nisingekuwa Harmonize pale niko. Unapata kuna fans wametoka mbali hadi Eldoret kwa sababu yake. Sometimes unafaa kuangalia mafans kwanza,” amesema Jaguar kwenye mahojiano yake kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio.

Kwa upande mwingine, Jaguar amesema kuwa amewasiliana na Promota huyo ambaye alimzingua Harmonize, lakini alichoambiwa ni kwamba Harmonize alikataa kulipwa kwa Ksh alitaka alipwe kwa mfumo wa Dola. Sikiliza mahojiano ya Jaguar kwenye kipindi cha Mambo Mseto.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents