BurudaniVideos

Jay Moe: Ni lazima nitakuja kufanya video ya Famous

Rapper Jay Moe amesema ‘Famous’ katika nyimbo zake zote, ndio wimbo ambao anajuta kwanini hakuwahi kuufanyia video.

13249930_815259015274264_92309098_n

Amesema katika nyimbo zake zote, Famous aliomshirikisha P-Funk Majani, bado anaendelea kuusikia ni mpya kila anapousikia. Moe ameongeza kuwa watu wengi hata leo wameendelea kumlaumu kuwa aliupoteza bure.

“Bado ukipigwa hadi leo unasound kisasa zaidi tofauti na kama nikisema nataka kushoot ‘Kama Unataka Demu’ kuna wengine siwezi kuwapata kirahisi, lakini Famous it’s just me and P-Funk na kuonesha tu hiyo lifestyle ya Famous guy inakuaje, kwahiyo tunataka tushoot hiyo,” Jay Moe aliiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Jay Moe amedai kuwa hata kama akiwa mzee lazima tu atafanya video ya Famous.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents