Je! Unafahamu? Diamond na Queen Darlin wanachangia Baba!

Kwa wale walioshuhudia ama kuiona mtandaoni show ya Diamond are Forever yake Diamond Platnumz watakumbuka kuwa mwanadada Queen Darling alikuwepo kunogesha show hiyo.

Lakini watu wengi mpaka sasa hawajui kuwa Diamond na Queen Darlin ni mtu na dada yake.

Wasanii hawa Baba yao ni mmoja. Damu ya mzee Abdul Juma ipo kwenye mishipa ya wakali hawa wa muziki wa Bongo Flava.

Ingawa hawajataka kuwa karibu zaidi kama inavyotakiwa kuwa, Diamond ambaye jina lake halisi ni Nasib Abdul na Queen Darlin aliyezaliwa kwa jina la Mwajuma Abdul Juma wanapendeza sana wakiwa kwenye stage moja.

Japo ngoma ‘Maneno Maneno’ ya Queen Darlin aliyomshirikisha Dully Sykes ilimrudisha tena kwenye ramani ya muziki kiasi cha kupata tuzo ya wimbo bora wa Dancehall katika tuzo za Kili, tunahisi Diamond anapaswa kufanya mengi zaidi kumpandisha zaidi dada yake.

Wakati mwingine kwakuwa wamekuzwa na mama tofauti huenda wamejikuta wakiishi mbalimbali katika maisha yao, lakini ukaribu wao kimuziki kama kaka na dada unaweza kuleta kitu kinachovutia zaidi kwa mashabiki wao.

Hata hivyo ni ngumu kuujua uhusiano kati ya ndugu hao nje ya maisha ya muziki lakini pata picha wakiwa karibu kama Ray J na Brandy ambao undugu wao ni karibu kiasi cha kuwafanya waonekane kama marafiki tu.

Related Articles

Back to top button