Burudani

JEURI YA PESA: Diamond kutumia mil. 150 kwenye Birthday ya Tiffah, Harmonize akifanya ‘shopping’ ya mil. 100 Afrika Kusini

Kwa sasa ukizungumzia wasanii wenye fedha nchini Tanzania huwezi kuacha kuwataja Harmonize na Diamond Platnumz, na hili linaonekana wazi hata kwenye matumizi yao ya kawaida.

Siku za hivi karibuni Diamond Platnumz ametangaza kuwapeleka watu 50 kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kati ya watu hao 30 ni mashabiki wake na 10 watakuwa ni wanakamati wa tukio ambao wataongozana na watoto wao.

Anyway! tupige mahesabu ya kawaida ya nauli ya mtu mmoja ya kwenda Afrika Kusini na kurudi kwa ndege. Kwa nauli ya chini ya daraja la Economy ni dola $600 sawa na  tsh milioni 1.350.000.

Ambapo ukizidisha kwa watu 50 utapata milioni 67.5.  Gharama za kuishi Afrika Kusini kwa siku tatu kwa watu 50 yaani kuanzia tarehe 17 hadi 19, 2018 kwa hoteli ya bei ya chini ni dola $150 kwa siku ambapo kila mtu kwa siku tatu atatumia dola $450 kwa ajili ya malazi, ambayo ni sawa na tsh 1.2 .

Ukipiga mahesabu ya kawaida ya kila mtu milioni 1.2 ya malazi kwa watu 50 unapata kama tsh milioni 60 na hapo bila gharama ya chakula. So roughly kuwagharamia watu 50, Diamond atatumia si chini ya milioni 150 kwa fedha ya kitanzania ili kukamilisha zoezi la kuwasafirisha watu 150 .

Wakati hayo yakijiri, msanii mwingine kutoka WCB, Harmonize yeye ameonekana akitumia fedha zake kwa matumizi mengine kabisa ikiwemo kununua nguo kutoka kwenye Clothing brand za gharama ya juu kabisa.

Harmonize unaweza ukasema ndio msanii kwa sasa Tanzania ambaye anafululiza kuvaa bidhaa za Gucci ambazo ni moja ya bidhaa za nguo zenye gharama kubwa duniani.

Tuanzie hapa! mwezi uliopita Harmonize alifanya shopping kwenye duka kubwa la bidhaa za Gucci nchini Afrika Kusini ambapo kwa kawaida hauwezi kuingia kwenye maduka hayo ya bidhaa za bei ghali duniani kama hauna dola $30,000 yaani zaidi ya tsh milioni 60.

Hii ndio maana hata baada ya kutoka kwenye duka hilo Harmonize mwenyewe alikiri kuwa bidhaa zao ni ghali sana ingawaje, ndio bidhaa azipendazo sana.

Tuanze na mahesabu ya kawaida kwa nguo alizonunua Harmonize kutoka Gucci, ambazo anazivaa kwa sasa hivi kwenye show yake.

T-shirt kama hiyo unayoiona ameivaa Harmonize kwenye picha akitumbuiza inauzwa kwa dola $980 ambayo ni sawa na Tsh milioni 2.2 za kitanzania.

Soksi za Gucci alizovaa Harmonize kwenye hiyo picha zinauzwa dola $120 kwa pea moja ambayo ni sawa na tsh 273,000/= .

 

Viatu vya Gucci alivyovaa kwenye hii picha vinauzwa dola $650 ambayo ni sawa na Tsh milioni 1.4, Track suti full ni dola $1,490 ambayo ni sawa na Tsh milioni 3.3 .

Kwa maana hiyo picha hiyo unayoiona juu Harmonize akitumbuiza mavazi yake kwa ujumla ni dola $2,260 ukijumlisha na saa ambayo inauzwa dola $1,020 unapata dola $3,280 ambayo ni sawa na tsh milioni 7.4 .

.

Ukweli ni kwamba Harmonize hana nguo moja au mbili za Gucci kwani karibia show zake zote huwa anabadilisha mavazi hivyo ni uhakika kuwa kwa sasa huenda akawa ni moja ya wasanii wanaovaa nguo za bei ghali zaidi ila sio kupendeza ukimtoa Diamond Platnumz.

Narudia tena Harmonize ni moja ya wasanii wanaovaa nguo za bei ghali zaidi nchini Tanzania ila sio msanii anayependeza zaidi kwani kuvaa kitu cha gharama sio  ndio kupendeza.

Faida ya kuvaa nguo hizo za gharama zaidi duniani kwa yeye kama msanii:

Bila ubishi kwa msanii kuvaa nguo za brand za bei kubwa kama Gucci, Louis Vuitton, Chanel, Versace, Balmain, Dolce and Gabbana na Hermès ni moja ya njia ya kujibrand hususani kwa wasanii wa Afrika.

Hujawahi kufikiria, labda P. Diddy amekutana na Harmonize halafu kamkuta na muonekano huo akiwa ametupia bidhaa za Gucci bila shaka utambulisho wake utakuwa wa maana zaidi.

Wizkid akiwa ametupia bidhaa za Gucci hapo kwa mahesabu ya kawaida ni zaidi ya Milioni 10 za kitanzania.

Pia ni status kwa msanii kuvaa nguo ambazo ni nadra kuwakuta watu wa kawaida wakiwa wamevaa, kumbuka utofauti wa muonekano wa kimavazi ni muhimu sana kwa wasanii.

Bei zote zilizotajwa hapo juu ni kwa mujibu wa mtandao wa gucci.com ambapo hazishuki wala kupanda duniani .kote.

Related Articles

39 Comments

  1. Uyo harmonize angekua nayo hyo milion Mia c angeenda kumjengea bibi yake nyumba mtwara uko achen kupaisha watu wakt hawajawa na uwezo huo…shopping milion Mia NAKOJOA. ..HARMO HUYU TUNAEMJUA? ?

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents