HabariMichezo

Jina la Haji Manara lafikishwa mezani kwa pilato

Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefungua shauri mbele ya Kamati ya Maadili dhidi ya Ofisa wa Klabu ya Yanga, Haji Manara kutokana na vitendo vya ukiukaji wa maadili.

Kamati ya Maadili kupitia kwa Mwenyekiti wake tayari imepewa taarifa kuhusu malalamiko dhidi ya Manara, hivyo itapanga siku ya kusikiliza shauri hilo na Mlalamikiwa atapewa taarifa.

TFF imewakumbusha wanafamilia ya mpira wa Miguu kuwa wanabanwa na Katiba na Kanuni mbalimbali za mchezo huo, hivyo wanatakiwa kuwa makini kwa vitendo na kauli zao kuhusu mpira wa miguu.

 

Related Articles

Back to top button