Habari

Joe Biden aongoza, avunja rekodi ya Barack Obama  (+Video)

Mwaka 2008, Barack Obama alipata kura 69,498,516 katika uchaguzi wa urais ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kutokea. Lakini kwa sasa mgombea urais kupitia Chama cha Democratic, Joe Biden ambaye pia aliwahi kuwa makamu Rais wa Obama amevunja rekodi hiyo kwa kupata 70,470,207  (asilimia 50.3) huku bado kura zikiwa zinaendelea kuhesabiwa.

Biden anaongoza kwa kura akimzidi mpinzani wake Rais Donald Trump ambaye mpaka sasa amejikusanyia kura 67,280,936 (asilimia 48.0) ikiwa ni mpaka leo Jumatano. Mchuano mkali bado unaendelea wa kuwania nafasi ya kuelekea Ikulu ya White House.

Mamilioni ya kura bado hayajamalizika kuhesabiwa mpaka sasa hivyo wagombea wote wawili wanayonafasi ya kuingia Ikulu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents