Burudani

Joh Makini aeleza kwanini hapendi kufananishwa na rapa wengine

Hitmaker wa Don’t Bother, Joh Makini amesema mashabiki na watu wanaopenda kuwafananisha rappers, ndio wanaosababisha kuwepo kwa ugomvu usiojenga tasnia ya muziki.

joh makini

Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Alhamisi hii, Joh amesema hali hiyo inawafanya wasanii wengine wajisikie wapo chini na kusababisha chuki.

“Sipendi kwa sababu mimi toka naanza muziki wangu kuna njia zangu ambazo napita. Sio kitu kibaya watu kufananisha kwa sababu si wote tunafanya Hip Hop,” alisema.

“Lakini wakati mwingine hivi vitu vinazua hata chuki, watu wengine hutengeneza picha ambazo ni tofauti. Kama wewe mwenyewe unaweza kuwa shahidi sisi kama Weusi hatujawahi kumuongelea msanii yeyote vibaya na kutengeneza chuki. Tunajaribu sana kukwepa hivi vitu kwa sababu tulishagundua havijengi industry bali vinabomoa. Sisi tunalenga zaidi kwenye kujenga na kuendelea kuibrand Hip Hop ya Tanzania kwenda kwenye level nyingine kibiashara,” ameongeza.

“Mimi ukiniambia mambo ya conscious au sio conscious siyajui. Mimi nafanya muziki kutokana na feeling yangu na ninavyoandika muziki wangu nakuwa conscious.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents