Burudani
Jose Chameleone amzawadia meneja wake gari mpya
Muimbaji Dr. Jose Chameleone wa Uganda amedhihirisha kuwa yeye ni boss anayejali wafanyakazi wake, kwa kumnunulia gari mpya meneja wake kama zawadi ya utendaji wake mzuri wa kazi.
Chameleone amemkabidhi bwana Nkuke Robert Jackson gari mpya aina ya Golf 5. Jackson ambaye anatimiza mwaka mmoja toka aanze kufanya kazi na Chameleone ametoa shukurani zake kwa kuandika:
“Good works deserve good rewards. I thank team for the ultimate gift 2015. A great artiste with a great heart just beat me this funky golf 5 thanks Chameleon.”
Source: Msetoea