Burudani

Juma Nature asema haya kuhusu wasanii wanaotumia unga

Jana ilikuwa ni siku ngumu, ya kishujaa na ya kukumbukwa kwa rapper Young Dee baada ya kuamua kuusema ukweli kuhusiana na tetesi za matumizi ya madawa ya kulevya.

13388569_1132649460091171_1422662606_n

Alikiri kuyatumia kwa mwaka na nusu na kwamba ameacha huku akiahidi maisha mapya na kupendeza zaidi akiwa tena chini ya uongozi wa label ya MDB.

Rapper Juma Nature ametoa maoni yake pia kuhusiana na matumizi ya madawa hayo.

“Kuna mambo ambayo nikijiuliza jibu sipati hivi ni kweli kuna wasanii wanakula mambo hivi, mbona sisi uhuni tumepitia lakini lakaya hii nimpya,” aliandika kwenye Instagram.

“Punguzeni kuiga wadogo zng jamii inawategemea…maana hatatukisema tuwaombeee kazi bure mtarudia tu! Kwani huyo anayewauzia anawashikia bastora ndg zng? Misijapendezwa namichongo famfa kujiendekeza banaaaaa,” aliongeza.

Matumizi ya madawa ya kulevya kwa wasanii yamekuwa hadithi isiyoisha huku Chidi Benz na Ray C wakiwa wahanga waliotawala zaidi headlines kwa sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents