Burudani

Young Dee anakuja na mpango wa kuelimisha vijana kuhusu athari za matumizi ya Madawa ya kulevya

Rapper Young Dee aka ‘paka rapa’ baada siku ya jana kukiri alikuwa anatumia Madawa na kulevya, anakuja na mpango maalum ambao utaweza kuwaelimisha vijana kuhusu athari za matumizi ya Madawa ya kulevya.
13398965_259931741052515_1071474077_n

Akiongea na waandishi wa habari Jumatano hii, Mkurugenzi wa label ya MDB ambayo inamsimamia msanii huyo, Max Rioba, alisema tayari wao kama uongozi unaandaa mpango maalum ambao utampa fursa rapa huyo ya kuwaelimisha vijana kuhusu athari za matumizi ya Madawa ya kulevya.

“Tuna project ambayo tunaifanyiakazi, ambayo ziwezi kuiweka wazi zaidi kwa sababu ni mapema,” alisema Max.

“Nina uhakika utakapofikia wakati wake yeyote yule ambaye anataka kuingia kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya atajiuliza mara mbilimbili, sisi tulimuonyesha Young Dee wasanii ambao wameathirika na Madawa ya kulevya, tukamuuliza unataka kuwa kama fulani? Ungependa kesho tuwe na press conference kwamba umekufa? Kwamba tulikuwa na msanii, kwa hiyo kupitia mtindo kama huu utabadili mawazo ya vijana wengi”

Rapa huyo alikiri kutumia Madawa ya kulevya kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents