Michezo

Juventus yatwaa taji la Serie A kwa mara ya 5 mfululizo

Klabu ya Juventus imeshinda Ubingwa wa Serie A huko Italy kwa mara ya 5 mfululizo.

Ushindi huo umekuja baada ya Timu ya Pili kwenye Ligi Napoli kufungwa 1-0 na AS Roma huko Stadio Olimpico Jijini Rome.

Juve-bingwa-1

Juve waliifunga Fiorentina Bao 2-1 na kuhitaji Pointi 1 tu ili kujihakikishia Ubingwa lakini kipigo cha cha Napoli kimehakikisha hawawezi tena kuikamata Juve huku Mechi zikibaki 3.

Juve-bingwa

Juve sasa wana Pointi 85 wakifuatiwa na Napoli wenye Pointi 73 na AS Roma wana Pointi 71.

Kwa kutwaa Ubingwa Msimu huu, Juve walionyesha umahiri mkubwa kwani hapo Oktobo 28 walikuwa Nafasi ya 12 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara wa Serie A.

Lakini baada ya hapo, Juve walishinda Mechi 24 kati ya 25 za Ligi zilizofuatia na kutoka Sare 1.

Katika Mechi hiyo Bao la ushindi la AS Roma lilifungwa Dakika ya 89 na Radja Nainggolan kutokana na ushirikiano mwema wa Mkongwe Totti, Pjanic na Mohamed Salah

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents