BurudaniWema Sepetu

Kajala aapa kutousahau msaada wa Wema Sepetu

Kajala Masanja amesema kuwa pamoja na kuwa hawana waelewano mazuri na rafiki yake wa zamani Wema Sepetu, hawezi kusahau wema aliomfanyia wa kumtolea shilingi milioni 13 kwenye huku yake miaka kadhaa iliyopita.

11190015_1379771655686754_1979496546_n

Kajala amesema hafikirii kuzirudisha fedha hizo kwa Wema ambaye amekuwa akieleza kujuta kuutoa msaada huo.

“Sio kwamba natamani kumrudishia milioni 13, kwa sababu mimi najua yeye alinisaidia kipindi mimi naHitaji na hakuna mtu yoyote alitokea kunisaidia kipindi hicho,” Kajala aliiambia Global TV.

“Kweli nashukuru mpaka kesho kwa sababu alitoa msaada ambao siwezi kuusahau hata kama tuna ugomvi kiasi gani. Sasa kwa sababu yeye alisaidia kwa moyo mmoja na akikaa akiongea anajuta kwanini alinisaidia kumlipia Kajala inakuwa inamfutia hata zile baraka alizozipata.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents