Burudani

Kanye West afunguka kuongeza watoto na Kim “Mungu ananitumia kufikisha ujumbe kwa wanadamu, Utajiri wote nimepata kwake”

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Kanye West amesema kuwa Mungu anamtumia yeye kufikisha ujumbe kwa binadamu na hata mafanikio anayoyapata yote yanatokakwa Mungu.

Image result for kanye west late late show"
Kanye West akiwa kwenye kipindi cha The Late Late Show.

Kanye West akihojiwa na James Corden kwenye kipindi cha The Late Late Show, Amesema kuwa Mungu ndiye aliyefanya hadi kampuni yake ya mavazi ya Yeezus kufanya vizuri kimauzo na kumfanya kuwa moja ya watu maarufu kuingiza mkwanja mrefu duniani kwa miaka mitatu mfululizo.

Mafanikio yote ninayoyapata ni kutoka kwa Mungu, Najua ananitumia kufikisha ujumbe kwa wanadamu ili waendelee kumuamini. Kwa mwaka jana niliiingiaza dola Milioni $115 lakini hadi mwaka unaisha nikamaliza na deni la dola Milioni $35. Mungu alivyokuwa mkubwa baada ya kufungua huduma yangu ya kiroho ya kila Jumapili mwanzoni mwa mwaka huu, Nikaingiza dola Milioni $68. Kwa sasa Kampuni yangu ya Yeezus ni kampuni namba moja kutafutwa zaidi duniani kwenye mtandao wa Google. Ndio hayo ni mafanikio makuwbwa kutoka kwa Mungu.” amesema Kanye West.

Kanye West ambaye alialikwa na kwaya yake kwenye kipindi hicho, Alizungumzia pia familia yake akiwemo mke wake Kim Kardashian na jinsi Mungu alivyoibariki familia yake.

Watu walisema tutashindwana, Siwezi kuwa na Kim kwa sababu wote ni mastaa, Lakini mpaka sasa tupo safi na tumepata zawadi ya watoto,“amesema Kanye na kuulizwa swali na Cordon kama angependa kuzaa watoto wangapi.

SWALI: Ungependa kuongeza watoto labda watano au sita, “Natamani wafikie 7, Tulishapanga na mke wangu (Kim).“.

Kwa sasa Kanye West na Kim Kardashian wana watoto wanne, Psalm West, North West, Chicago West na Saint West.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents