Burudani

Kanye West ashiriki kwenye auditions za shindano la kusaka vipaji ‘American Idol’!

Katika hali ya kushangaza, mtangaza nia ya kugombea urais wa Marekani 2020, rapper Kanye West weekend iliyopita aliamua kupitia sehemu zilipokuwa zinafanyika auditions za shindano la kusaka vipaji ‘American Idol’ jijini San Francisco, na kuchukua namba ya ushiriki kisha kwenda mbele ya majaji na kuonesha kipaji chake, lol!

Kanye AI-2

Majaji wa shindano hilo Jennifer Lopez,Harry Connick, Jr. na Keith Urban walishikwa na mashangao walipomuona Kanye akiwa na tiketi yake ya ushiriki, ambapo J.Lo alisikika akiuliza “Is that Kanye West?” mara baada ya kumuona akiingia.

Kanye AI

Kanye aliimba wimbo wake mwenyewe “Gold Digger”.

Kim Kardashian pia alikuwepo nje ya chumba cha usaili kumsindikiza mumewe na kushare tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuandika ‘Surprise’.

kanye-idol-1

Bado haijafahamika kama ilipangwa kama publicity stunt ya kuongeza ratings za kipindi ama ilikuwa ni sehemu ya kuongeza tu burudani.

Tazama ilivyokuwa
https://youtu.be/fpeLy_0Ulpw

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents