Burudani

Kanye West na Drake waweka kambi milima ya Wyoming

Habari za kuaminika zinaeleza kuwa rapper Kanye West yupo katika maandalizi ya albamu yake ijayo huku moja ya ngoma itakayopatikana katika albamu hiyo itamuhusisha mkali wa ‘God Plan’ Drake.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, imeelezwa kuwa Drake yupo katika milima ya Wyoming inayopatikana Magharibi mwa Marekani.

Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa watu hao wamekuja na vifaa mbalimbali vya kurekodia muziki, kitu kinachowafanya waamini kuna midundo mikali inakuja katika albamu mpya ijayo ya 19 iliyowakutanisha wakali kama:-Travis Scott, The Dream, Lil Uzi Vert, Kid Cudi, Nas na wengineo wengi.

‘Life Of Pablo’ ni albamu ya 18 ya rapper huyo iliyotoka mwaka 2016 iliyokuwa na jumla ya ngoma 19. Pia ilikuwa album ya kwanza iliyotoka mtandaoni na kwenda platinum, kwa uthibitisho wa Recording Industry Association of America, RIAA. Vile vile ilivunja rekodi kwa kusikilizwa mara milioni 250 mtandaoni, siku 10 tangu iwekwe kwenye mtandao wa Tidal.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents