Burudani

Uzuri wangu wakati wote mademu wamenizunguka – Prezzo

Rapper kutoka nchini Kenya, Prezzo amejibu kuhusu tetesi za kuchana na aliyekuwa mpenzi wake Amber Lulu.

Prezzo ambaye kwa sasa yupo Tanzania kwa ajili ya promotion ya ngoma yake na Dogo Janja ameiambia FNL ya EATV kuwa kuachana kwao ni baada ya Amber Lulu kumuona na wanawake wengine bila kujua ukweli wa ukaribu wao ila bado anampenda.

“Uzuri wangu mimi huwa na mademu wakati wote wamenizunguka, shida nyingine mtu akiniona na demu fulani labda ni dada au binamu yangu kwa sababu mimi nina familia Tanzania tayari ni kosa,” amesema Prezzo.

Soma Pia; Usimfananishe mume wangu (Prezzo) na Young Dee – Amber Lulu

Licha ya kauli hiyo ya Prezzo bado wawili hao wameonekena wakiwa pamoja kwenye mitandao ya kijamii, siku ya jana Amber Lulu katika ukurasa wake wa Instagram alipost picha wakiwa pamoja na kuandika; ‘Napenda nnyaa kama Mende ilo tendo tulitendee #hamsamia’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents