Burudani

Karrueche awagombanisha Chris Brown na Soulja Boy

Mwaka 2017 umeanza vibaya kwa Chris Brown na Soulja Boy – kwakuwa wameanzisha bifu chanzo kikiwa ni mrembo Karrueche Tran.

Tangu alipoachana na Karrueche Chris amekuwa akimfuatilia mrembo huyo huku mara kadhaa akigombana na wanaume ambao wanaomtolea udenda. Na sasa balaa limemkumba rapper Soulja Boy baada ya kulike picha ya mrembo huyo kwenye mtandao wa Instagram kitendo ambacho kimeonekana kumkera Brown.

Soulja Boy amefunguka kupitia mtandao wa Twitter kuwa Chris amemtafuta na kumpiga mikwara baada ya kulike picha hiyo.

Chris Brown amekuwa akijaribu mara kadhaa kutaka kurudiana na Karrueche lakini imekuwa ngumu kwa mrembo huyo kukubali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents