Habari

Katy Perry azitosa dola milioni 20 za American Idol


Kama Katy Perry angesema “Yes” kwa American Idol angelipwa pesa nyingi kumzidi hata Mariah Carey.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Us Weekly kuwa watayarishaji wa show hiyo walikuwa na hamu ya kumpata muimbaji huyo mwenye miaka 27 kujiunga na panel ya majaji na kumpa dau la dola milioni 20 kwa mwaka.

Bahati mbaya ni kuwa amelikataa dau hilo na hivyo waandaaji wa show hiyo wameendelea na msako wa kutafuta majaji wengine watakaoziba mapengo ya Jennifer Lopez, Steven Tyler na Randy Jackson (ambaye ataondoka kwenye kiti cha majaji na kuwa mwalimu kwenye show ijayo).

Majina kadhaa yameendelea kutajwa kuwa majaji wapya akiwemo Nicki Minaj, Pharrell Williams, Keith Urban na Nick Jonas japo wote hawajathibitishwa.

Mwishoni mwak July, Mariah Carey alisaini rasmi kuwa jaji wa shindano hilo kwa dau la dola milioni 20 na kumfanya kuwa jaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye mashindano ya aina hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents