Burudani

‘Kazi yake Mola’ ni funzo tosha kwa wasanii – Madee

Rapa kutoka kundi la Tip Top Connection, Madee amefunguka na kusema kuwa wimbo wake wa ‘Kazi yake Mola’ ni wimbo ambao ni funzo tosha kwa wasanii wa muziki hapa nchini Tanzania ambao wanatoa nyimbo zinazodumu miezi mitatu tu kwa kusikilizwa.

Image result for Madee

Madee amesema wasanii wengi kwa sasa wanatoa nyimbo ambazo zinasikika miezi mitatu tu na baadae kupotea kabisa lakini wimbo wake wa kazi yake mola ni wimbo ambao utaendelea kusikilizwa miaka yote kwani ujumbe wake ni mzito na unadumu.

Nadhani Kazi yake Mola ni funzo tosha kwa wasanii wa muziki hapa Bongo,ni wimbo ambao hata nikifa leo bado utaendelea kusikika kwani ujumbe wake ni mzito na unadumu kwenye maisha ya kawaida,Nasema ni somo kwa sababu wasanii wengi siku hizi nyimbo zao hazidumu yaani miezi mitatu tu ngoma imeshachoka,Hivyo nawashauri wajifunze kupitia Kazi yake mola“Alisema Madee kwenye mahojiano yake na Bongo Five.

Aidha,Madee ametoa pole kwa Ndugu,Jamaa na marafiki wote waliopatwa na msiba huko mkoani Arusha kwenye ajali ya gari iliyoua wanafunzi 32,Walimu 2 na dereva mmoja wote wa Shule ya Lucky Vicent.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents