Burudani

Millard Ayo asimulia alivyonusurika kwenye ajali kama iliyoua 32 Arusha (Video)

Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Millard Ayo wakati akitoa salamu zake za rambirambi kufuatia vifo vya wanafunzi 32, walimu 2 pamoja na dereva mmoja, amefunguka kuzungumzia namna alivyonusurika kwenye ajali kama hiyo akiwa mdogo.

Katika ajili hiyo ambayo amedai ilitokea mwaka 1994 mkoni Arusha Ngorongoro, ilisababisha vifo vya wanafunzi wenzake  wanne ambao alikuwa nao kwenye safari hiyo ya kuelekea Serengeti.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Millard Ayo amedai katika ajali hiyo alimpoteza rafiki yake ambaye alikaa naye siti moja.

“Pole sana kwa familia za Arusha najua ni kiasi gani sasa hivi watu wana huzuni sana, watu 32 kwa wakati mmoja ni kitu kikubwa sana,” alisema Millard.

“Na mimi hii ajali nilipoisikia tu ni wanafunzi imenikumbusha mbali sana kwa sababu hata mimi mwenyewe niliwahi kupata ajali kama hiyo mwaka 1994 tulikuwa Ngorongoro sehemu moja maarufu inaitwa Malanja Cross. Tulikuwa na gari la jeshi wanafunzi wa shule ya msingi, Patandi Primary Schools Tengeru Arusha tukielekea Serengeti kuangalia wanyama lakini bahati mbaya gari ikafeli breki ikaingia bonde la ufa, wakafa wanafunzi wenzangu wanne akiwemo rafiki yangu ambaye nilikaa naye siti moja,” aliongeza Millard.

Mtangazaji huyo amedai yeye wakati basi hilo likibiringika, alikuwa amebanwa na chuma kichwani hivyo hakuweza kutoka mpaka watu walivyokuja kumwokoa.

Pia amesema aliumia vibaya katika mguu wake wa kushoto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents