Burudani
Kim Kardashian na kanye West watoa jina la mtoto wao wa tatu
Baada ya kusubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki jina la mtoto wa tatu wa couple ya mastaa maarufu duniani Kanye West na mkewe Kim Kardashian, hatimaye wazazi hao wametoa jina.
Kupitia mtandao wa Twitter wa Kim amethibitisha kuwa mtoto wao huyo wa kike aliyezaliwa mapema wiki hii na mama mwingine ambaye walimlipa ili awabebe mimba, wamemuita jina la Chicago West au ukipenda unaweza kulifupisha kwa kumuita Chi. Je unalionaje jina hilo?
Chicago West. https://t.co/3MyLwcIzTh
— Kim Kardashian (@KimKardashian) January 19, 2018
Chicago ameungana na ndugu zake wengine wawili akiwemo dada yake North mwenye miaka minne na kaka yake Saint West mwenye miaka miwili.