Habari

Kirusi kipya ni hatari, WHO chakipa jina Omicron

Shirika la afya duniani (WHO) limetangaza aina mpya ya kirusi cha corona kuwa “ya kutia hofu” na kuipatia jina Omicron.

Kina orodha ndefu ya mabadiliko ya kimaumbile, na tayari Ushahidi unaonyesha kuongezeka kwa hatari ya ongezeko la maambukizi mengine kuambukiza tena, imesema WHO.

Kwa mara ya kwanza aina hii iliripotiwa kwa WHO kutoka Afrika Kusini tarehe 24 Novemba, na imebainika pia katika mataifa ya Botswana, Ubelgiji, Hong Kong na Israeli.

Nchi kadhaa duniani sasa zimeamua kuweka marufuku au kuweka masharti ya usafiri wa kutoka au kuelekea nchini Afrika Kusini.

Wasafiri kutoka Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe, Lesotho na Eswatini hawataweza kuingia nchini Uingereza isipokuwa kama watakuwa ni raia wa Uingereza na Ireland au wakazi wa Uingereza.

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa safari za kutoka Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Namibia, Lesotho, Eswatini, Msumbiji na Malawi zitazuiwa, uamuazi huu ukiwa ni sawa na ule uliochukuliwa awali na Muungano wa Ulaya (EU). Hatua hii itaanza kutekelezwa kuanzia Jumatatu.

Brazil na Australia pia zimeanzisha masharti ya usafiri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents