Kisa kikombe cha Kahawa, Marubani wasimamishwa kazi
Tukio hilo lilitokea ndani ya ndege ya SpiceJet
Shirika la ndege la kibinafsi la Indialimewazuia marubani wake wawaili kutoendesha ndege kwa madai ya kuwa na kahawa na peremende ndani ya chumba cha rubaniili hali ndege ikiwa safarini angani
Tukio hilo lilijulikana baada ya picha ya kikombe kilichokuwa kimewekwa kwenyemtambo wa uongozaji wa ndege ya SpiceJet kusambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema wiki hii.
Taarifa zilisema kuwa ndege hiyo ilikuwa ikisafiri umbali wa futi 37,000wakati picha hiyo ilipochukuliwa.
Picha hiyo iliibua malalamiko , yaliyosababisha taasisi ya udhibiti wa safari za anga ya India kutoa onyo kwa ndege.
Jumatano SpiceJet ilisema kuwa inachunguza suala hilo, na imewasimamisha kazi marubani wanne, ambao wanadaiwa kuchukua picha hiyo, wakiwa mapumzikoni.
“Hatua inayostahiki zitachukuliwa dhisi yao baada ya kukamilika kwa uchunguzi,” alisema msemaji wa kampuni hiyo katika mazungumzo na gazeti la The Times la India.