AfyaHabari

Kobe Diego astaafu baada ya kuzaa watoto 800

Kutana na Kobe, Diego kutoka kisiwa cha Galápagos ambaye amejizoelea umaarufu mkubwa baada ya kuzaa Watoto 800 kuokoa viumbe vyake dhidi ya kutoweka.

Diego ‘mstaafu’ mwenye umri wa miaka 103 alikuwa sehemu ya mpango wa kuzaliana katika kisiwa cha Santa Cruz, Ecuador kwa miongo kadhaa kabla ya kuachiliwa ili aishi siku zake zote katika kisiwa alichozaliwa, Española.

Pongezi nyingi zimekwenda kwa Kobe, Diego baada ya kuzaa idadi kubwa ya watoto 40% ya kobe 2,000 ambao sasa wanaishi kwenye kisiwa hicho, na kumletea sifa kwa mchango wake mkubwa katika maisha ya viumbe vyake.

Diego ana uzito wa 80kg, urefu 90cm na urefu wa 1.5 mita kama atanyoosha miguu na shingo yake.
Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents