Michezo

Kocha wa Algeria ajiuzulu baada timu yake kufanya vibaya

Baada ya kutolewa kwa kikosi chake kwenye hatua ya makundi ya michuano ya mataifa ya Afrika, AFCON 2017, kocha wa timu ya taifa ya Algeria George Leekens ameamua kujiuzulu.

Leeken ambaye ni raia wa Ubelgiji amesema amemua kwa moyo mkunjufu kuacha nafasi hiyo, bila ya kushinikizwa.

“Kwa nia njema kabisa nimeamua kuacha ingawa nafanya hivi kwa uchungu moyoni, na naitakia kila kheri timu ifanye vyema kimataifa”. Aliandika kocha huyo kwenye tovuti ya AFF.

Alikabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo mwezi Oktoba mwaka jana (2016) akitokea klabu ya Lokeren ya Ubelgiji ambako alikwenda baada ya kuachana na timu ya Taifa ya Tunisia aliyoinoa kwa miaka miwili yaani 2014 na 2015.

Algeria walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo, imemaliza nafasi ya tatu katika kundi B, ikifungwa mechi moja dhidi ya Tunisia, na kutoka sare na Zimbabwe na Senegal.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents