Michezo

Konta ajitoa katika michuano ya Charleston

Mcheza tenisi raia wa Uingereza, Johanna Konta amejiondoa katika mashindano ya tenisi ya wanawake ya Charleston yaliyoanza Jumatatu hii kutoka na kuwa na maumivu ya bega .

Konta ambaye ana umri wa miaka 25 alikua mwingereza wa kwanza kushinda taji la michuano ya wazi ya Miami kwa kumfunga Caroline Wozniacki jumamosi iliyopita.

Mchezaji huyo amesema “Michuano ya Charleston ni mashindano makubwa nilitarajia kushiriki lakini nilikua nikipambana na maumivu haya toka kwenye michuano ya Miami kuanzia mwanzo hadi mwisho

Mmarekani Madison Keys anayeshikilia nafasi ya 11 kwa ubora wa mchezo wa tenesi kwa wanawake duniani ndie mchezaji pekee anayesalia katika michezo hiyo akiwa na kiwango cha juu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents