Habari

Korea Kusini yaitaka China kuidhibiti Korea Kaskazini

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol ameitaka China “kujitwika dhima kubwa zaidi” katika kupunguza uchokozi wa Korea Kaskazini kupitia mradi wake wa silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu.

Ofisi ya rais Yoon imearifu kwamba kiongozi huyo ametoa mwito huo alipofanya mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana na rais Xi Jinping wa China pembezoni mwa mkutano wa kilele wa kundi la mataifa ya G20 unaofanyika Indonesia.

Wakati wa mazungumzo hayo rais Yoon aliweka wazi wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa mivutano kwenye rasi ya Korea na kuelezea matumaini kwamba China itatumia ushawishi iliyonao kuidhibiti Korea Kaskazini.

Kwa upande wake rais Xi amesema China inaunga mkono juhudi zote za amani baina Korea mbili na iko tayari kusaidia mpango wa kuondoa silaha nzito kwenye kanda hiyo iwapo pande zote zitakuabliana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents