BurudaniHabari

Love Damini ya Burna Boy ndani ya listi tuzo za Grammy

Listi ya wasanii wanao wania tuzo za Grammy mwaka huu zimetolewa hapo jana siku ya Jumanne Novemba 15.

Staa wa muziki kutoka Nigeria Burna Boy ameingia kwenye kinyang’anyiro hicho kupitia albame yake ya Love Damini kipengele cha muziki wa Kimataifa.

Burna Boy anawania pamoja na Berklee Indian ensemble, Angelique Kidjo na Ibrahim Laalouf, Masa Takumi, Anoushka Shankar.

Muimbaji mashuhuri wa Marekani, Beyonce, anaongoza katika orodha ya wateule wa tuzo za Grammys, akiingia kwenye vipengele tisa na kuongoza, Kendric Lamar akiwa kwenye vipengele nane, Adele kutoka Uingereza akiwa kwenye vipengele saba, Brandi Carlile vipengele saba.

Baadhi ya wale waloteuliwa kunangania tuzo la albumu ya mwaka ni pamoja na Kendric Lamar, Adele, Brandi Carlile, Lizzo, Bad Bunny, Mary J Blige, HarryStyles, Abba, Coldplay na Beyonce. Utambuzi na uteule wa Beyonce unafwatia kutowa kwa albamu yake kabambe yenye miondoko ya disco ijulikanalo kama “Renaissance”. Albamu liitwalo” Mr. Morale And The Big Steppers, la Kendik Lamar, Adele nae na albamu lake 30 nae Brandi Carlile na albamu lake, In These Silent Days. Waimbaji hawa wanne kadhalika nyimbo zao zimeteuliwa katika kundi la rekodi ya mwaka. Wimbo wa Adele, Easy On Me, ulitia fora sana hapo mwaka jana.

Katika kundi la msanii mpya bora, bado haiko bayana nani ataibuka mshindi, lakini baadhi ya wale waloteuliwa ni waimbaji, Anitta, Omar Apollo, Latto, Samara Joy, Tobe Nwigwe , Molly Tuttle miongoni mwa wengine wengi.

Katika miondoko ya Rap, Dj Khaled akishirikiana na Rick Ross, Lil Wayne, Jay Z, John Legend na Fridayy wanaongoza katika kundi la album bora la Rap, na wimbo “God Did”. Wengine waloteuliwa katika kundi hilo ni pamoja na Jack Harlow, Future, Pusha T na Kendrik Lamar.

Kundi la mziki bora wa Reggae, limeongozwa na Kabaka Pyramid na wimbo The Kalling, Koffee na wimbo wake Gifted, Sean Paul na wimbo wake Scorcha na Shaggy, akiwa amerudi tena kwenye mziki baada ya kupotea kwa mda, na wimbo wake, Com Fly Wid Mi.

Tuzo za Grammays za mwaka 2023 zinatarajiwa kufanyika Februari 5, 2023 katika ukumbi wa Crypto.com mjini Los Angeles nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents