Michezo

Kuelekea UEFA, Mourinho awachana wachezaji wake ‘Kama unapresha baki nyumbani, tazama kupitia luninga’

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amewaambia wachezaji wake kuwa ni vyema wakabaki nyumbani na kuitazama timu hiyo kupitia luninga kama hawawezi kuzizuia presha zao wanapocheza Old Trafford

Jumamosi iliyopita imeshuhudiwa United ikilizamishwa sare nyumbani dhidi ya Crystal Palace matokeo yanayoleta tafsiri ya timu hiyo kuwa imeshinda michezo mitatu pekee kati ya tisa iliyocheza kwenye dimba la Old Trafford kwa mashindano yote msimu huu.

Katika michezo miwili ya ufunguzi ya Champions League kundi ‘H’ ikiwa nyumbani United ilitoka sare na Valencia huku ikifungwa na Juventus.

‘‘Kama unahisi unapresha baki nyumbani na ninaposema nyumbani simaanishi uwanjani, na sema nyumbani, nyumbani na utazame kwenye luninga,” amesema Mourinho.

‘’Wakati watu wanapokuja kutusapoti huwa sijiskii presha hasa kucheza kwenye uwanja wa nyumbani.”

‘’Nafikiri itakuwa ni upungufu wa heshima kwa uwanja wetu na mashabiki kwa ujumla kusema tumejiandaa kwaajili ya ugenini badala ya nyumabani.”

Miamba hiyo ya soka ya Uingereza leo siku ya Jumanne inakibarua cha kuwakabili Young Boys kwenye michuano hiyo huku ikihitaji ushindi ili kukwepa kuweka rekodi katika historia ya timu hiyo ya kucheza michezo mitatu ya Ulaya kwenye dimba la Old Trafford pasipo kufunga hata mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents