Technology

#Kumbukizi: Faustine Ndugulile – Tulikuwa hatuna bei elekezi za bando, hizi ndio bei za bando mpya (+ Video)

“Nilipoingia katika wizara hii jambo ambalo nilisema ndani ya siku 100 lazima nilitatue ni suala la Bando, malalamiko yalikuwa ni mengi, na nimetumia nguvu nyingi sana kuhakikisha hili jambo tunalikamilisha haraka”

“Inawezekana katika matangazo yetu wananchi hawajaweza kuyaelewa vizuri, maswali yote kuhusu bando tumeweza kuyapatia majibu, tangu tumeingia kwenye wizara hii tulikuwa hatuna bei elekezi ya vifurushi vya bando, kama ilivyo kwenye mafuta na umeme”

“Kwa sasa hivi tumetoa bei elekezi ya Data itaanzia shs 2-9 kwa MB 1 kuanzia April 2, makampuni ya simu hayapaswi kuendelea zaidi ya hapo na yanatakiwa yazingatie bei hiyo”

“Hakuna upandishaji holela wa Bando mpaka baada ya miezi mitatu ipite”

“Kampuni hazitaruhusiwa kupunguza spidi ya bando, kampuni inakupa GB 10 halafu inaminya spidi ya bando”

“Na sisi kama Serikali tuna mifumo ya ku ‘monitor’ performance ya kampuni za simu nimetoa maelekezo kila baada ya miezi mitatu watakuwa wanatoa taarifa, makampuni yote ya simu yameshindwa kutoa huduma bora kwa wateja, na nimesema kila kampuni ya simu ifanye Uwekezaji wa kutoa wa kutoa huduma kwa wananchi na wapate kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, tumewapa muda wa miezi mitatu wa kujipanga”

“Kama Mtu anataka kutumia kifurushi chake na muda wake unakaribia kuisha, akinunua kingine kile cha mwanzo kitaendelea kutumika” @faustine_ndugulile, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

 

Bofya hii link hapa chini kumsikiliza Waziri.

 

https://www.instagram.com/p/CNKNnjRFaBe/

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents