Burudani

‘Kupatwa kwa Jua’ kulivyoingiza msamiati mpya kwenye Kiswahili

Kipindi usafiri wa magari yaendayo kwa kasi umetambulishwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam, msamiati mpya wa Kiswahili ‘Mwendo kasi’ ulitambulishwa, si tu Dar, bali Tanzania nzima.

14156300_1637195106570399_1282830229_n

Mwendo Kasi, neno la Kiswahili lililokuwa likitumika mara nyingi tu kwenye mazungumzo ya wananchi wanaozungumza Kiswahili, liligeuka kuwa msamiati wa tofauti kabisa. Liligeuka kuwa ‘kivumishi cha sifa’ kinachotumika sana kwa sasa.

Kwa mfano, pale mtu anapotaka kuzungumzia mtu mnene kupitia kiasi, basi siku hizi humwelezea kama mtu mwenye ‘unene wa mwendo kasi.’ Ama kama kundi la watu limepigwa picha likila ugali mkuuubwa, basi ugali huo hutambulika kama ‘ugali wa mwendo kasi’ na mifano mingine kibao.

Wakati ambapo kivumishi hicho kikiendelea kutawala mazungumzo yetu, neno jingine tena limeingia rasmi wiki hii.

Kupatwa kwa jua ni tukio la nadra sana ambalo hutokea katika uso wa dunia. Baada ya miongo takriban minne iliyopita ambapo tukio hilo lilitokea mara ya mwisho na kuonekana nchini Aprili 18, 1977, limetokea Alhamis hii, Septemba 1.

Wakazi wa Rujewa, Mbeya walikuwa na bahati ya mtende ya kulishuhudia tukio hili kwa mtazamo wa ‘high definition’ HD! Wageni kutoka mataifa mengine nao walijumuika ngomani!

Sasa tukio hilo limemalizika na kuacha msamiati mwingine mpya ulioshika kasi tayari. Watu hawazungumzi tena kuhusu kupatwa kwa jua bali kupatwa kwingine kabisaaa!

Mfano wallet ambayo haina hata shilingi ndani yake basi hapo kuna kitu kinachoitwa ‘kupatwa kwa pochi.”

Kupatwa 1

Au pale watoto watundu wanapoivamia friji iliyojaa kila aina kilevi wakati wazazi hawapo, kinachotokea ni kupatwa kwa…

Kupatwa 3

Mifano mingine ni pamoja na:

Kupatwa 2

Kupatwa 4

kupatwa 5

Pamoja na yote hayo, ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa hai katika tukio hilo la maajabu ya ulimwengu na la kihistoria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents