Kylian Mbappe hauzwi – Msimamo wa PSG

Afisa Mtendaji Mkuu wa matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain, Nasser Al-Khelaifi amesema mabingwa hao wa Ligi 1 hawatamuuza mshambuliaji wao Kylian Mbappe, 22. (AS – in Spanish)

Kuhusiana na tetesi za kuhusishwa na mchezaji wa Barcelona Lionel Messi, Rais huyo wa PSG, Nasser Al-Khelaifi amesema wachezaji bora wote wanataka kujiunga na klabu yetu, hata hivyo amekataa kutolea ufafanuzi juu ya tetesi hizo za nyota wa Barcelona, Lionel Messi.

Messi amekuwa akihusishwa na miamba hiyo ya soka kutoka Ligi 1.

Aston Villa wako tayari kumnunua kiungo wa kati wa Southampton na England James Ward-Prowse, 26, siku moja baada ya kukubali kuvunja rekodi ya usajili wa klabu hiyo kumsaini kiungo wa kati mwenzake Emiliano Buendia kutoka Norwich. (Guardian)

Itagharimu euro milioni 200 sawa na (paundi milioni 171.8) kumnunua mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kutoka Borussia Dortmund msimu huu. (AS – in Spanish)

Erling Braut Haaland

Wolves wnajiandaa kupokea ofa ya Arsenal wiki hii kuhusiana na kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 24. (Mail)

Barcelona wamefufua tena mpango wa kumsaka mlinzi wa Manchester City Mhispani Aymeric Laporte, 27, na huenda wakamtoa Sergi Roberto, 29, kama sehemu ya kufanikisha mkataba. (Sport – in Spanish)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, bado huenda akajiunga na AC Milan, licha ya Chelsea kutangaza mpango wa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja wiki iliopita. (Goal)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud,

Barcelona wameamua kutoongeza ofa ya Georginio Wijnaldum, 30, baada ya Paris St-Germain kuongeza mara mbili marupurupu ya ofa iliyotolewa na Barca. Kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, ambaye yuko huru kuondoka Liverpool,anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitatu na PSG. (Fabrizio Romano, Twitter)

Juventus huenda wakajaribu hatua sawa na hiyo na mchezaji mwingine wa anayelengwa na Barcelona, mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 27, ambaye anajiandaa kuondoka Lyon kwa uhamisho wa bure. (Mundo Deportivo)Memphis Depay

Real Betis wamepiga hatua katika mazungumzo yao na mlinzi wa Paraguay Fabian Balbuena, 29, ambaye mkataba wake katika klabu ya West Ham inaelekea kumalizika. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Tottenham itathibitisha uteuzi wa mkufunzi wa zamani wa Juventus Fabio Paratici msimu huu, baada ya juhudi zao za kumpata mkufunzi wa zamani wa-Juve na Inter Milan Antonio Conte kugonga mwamba. (Mirror)Antonio Conte

Lazio huenda wakamsajili meneja wa zamani wa Juventus na Chelsea Maurizio Sarri, 62, kama mkufunzi wao mpya wiki hii. (Corriere dello Sport – in Italian)

Related Articles

Back to top button