Siasa

Rais Samia Suluhu kukutana na Wanawake mkoani Dodoma

Wanawake zaidi ya 10,000 Mkoa wa Dodoma makundi mbalimbali wanatarajiwa kukutana na Rais  Samia Suluhu Hassan Juni 8 mwaka huu katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Hayo yamesemwa leo Juni 6,2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma,  amesema Rais Samia atazungumza na wanawake wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya kina mama wa mikoa yote.

Wakina mama kwa uwakilishi wao wa makundi mbalimbali kutoka wilaya za Dodoma na maeneo ya karibu wamepewa mwaliko wa kushiriki kwenye mkutano huo,” amesema Mtaka.

Aidha, ametaja makundi hayo kuwa ni pamoja na wabunge wanawake bila kujali wapo chama gani, madiwani na makundi kama wajasiriamali, mama ntilie na kila aina ya kina mama watapata nafasi ya kuwakilishwa na wenzao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents