MichezoUncategorized

Leo tutaonyesha kuwa tunaweza kushinda,tutavunja rekodi ya miaka minne – Pochettino

Leo tutaonyesha kuwa tunaweza kushinda,tutavunja rekodi ya miaka minne - Pochettino

Kocha mkuu wa klabu ya Tottenham hatspurs na raia wa Argentina Mauricio Pochettino ameahidi kuivunja rekodi yao mbaya katika uwanja wa Old Trafford kwenye mchezo wao wa leo usiku dhidi ya wababe hao wa Uingereza.

Tottenham wanakutana na Manchester United katika mchezo wa 53 wa ligi kuu nchini Uingereza katika uwanja wa Old Trafford huku Spurs wakiwa na rkodi mbaya dhidi ya mabingwa hao wa mara 20 wa ligi hiyo,wakifungwa na United katika michezo 33 na wao wakishinda michezo 8 huku sare zikiwa 11.

Licha ya Spurs kuonekana kuonekana wako vizuri mwanzoni mwa ligi kwa kushinda michezo yao miwili huku United akishinda mchezo mmoja tu,na kwa upande wa timu hizi mbili Spurs hajawahi kushinda katika uwanja wa Old Trafford unaomilikiwa na United tangu mwazo wa mwaka 2014 ikitimiza miaka minne hadi hivi sasa lakini sio Spurs tu bali ni kwa vilabu vinavyotoka London.

Pochettino, anahisi kuwa ni muhimu sana wachezaji wake kuonyesha kwamba wanaweza kupata matokeo nyumbani mwa United baada ya kipindi cha miaka nne.

Muargentina huyo amezungumza hayo wakati anafanyiwa Interview na Sky sports na kusema “Ni muhimu sana kwetu kushinda kwa sababu baada ya miaka minne ya kushindana na kupambana vya nguvu pale hatukufanikiwa kwani tulipambana zaidi ili kutoshindwa,na tupata matokeo mazuri hatukufanikiwa, ni muhimu kwende huko katika mchezo wetu wa leo Jumatatu tukajaribu kushinda mchezo huu na kuonyesha kwamba tunaweza kumpiga Manchester huko kwao”.

“Najua itakuwa ngumu, bila shaka, kwa sababu Manchester ni timu kubwa na ina wachezaji wanaoaminika na wakiwa na mmoja wa mameneja bora duniani”

“Lakini ni changamoto kubwa na nikasema mwanzoni mwa msimu kuwa huu ulionekana utakuwa msimu mkali kati ya misimu yangu ya usimamizi tisa, miaka 10 iliyopita tangu nianze kazi”

Na nahisi mechi hii itakuwa na changamoto kubwa sana kwani tutakabiliwa na timu ambayo ni nzuri sana na kuwa na wachezaji wazuri wanaoaminika na bila shaka, kucheza na kushinda katika uwanja wa Old Trafford si rahisi”

“Lakini sisi tutawaonyesha heshima nzuri ya mchezo na tunakwenda huko kujaribu kushinda na kufanya vizuri kwa njia yetu nzuri. kama hatutacheza katika pafomansi yetu bora zaidi, itakuwa ni vigumu sana kushinda kwa sababu Manchester ni timu kubwa na nzuri sana. ”

 

By Ally Juma.

 

Related Articles

3 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents