Habari

Lil Ommy akwara tuzo ya ‘STAR QT’ mtangazaji bora 2019 barani Afrika, Ashinda tuzo mbili ndani ya mwezi mmoja

Mtangazaji wa kituo cha radio cha Times FM, Lil Ommy ameshinda tuzo ya Star QT kwenye kipengele cha Mtangazaji Bora wa mwaka 2019 barani Afrika.

Tuzo za Star QT zimetolewa usiku wa kuamkia jana, Katika ukumbi wa The Edenvale City jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Lil Ommy

Akizungumzia tuzo hiyo, Lil Ommy ‘The MVP’ ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani, Amesema tuzo za Star QT ni tuzo kubwa sana kwake, Kwani zimetolewa kwa mwaka wa sita sasa na kuwashukuru mashabiki wake waliompigia kura.

Nashurukuru sana mashabiki wangu, Media na Wafanyakazi wenzangu. Kiukweli umekuwa ni mwaka mzuri kwangu hii ni tuzo yangu ya pili ndani ya mwezi huu (Oktoba). Kwa sasa nipo Marekani ila leo naanza safari nadhani Jumatano nitakuwa Bongo,“amesema Lil Ommy.

Lil Ommy ameshinda tuzo mbili ndani ya mwezi Oktoba, Zote ni tuzo za Mtangazaji Bora barani Afrika kwa 2019 akiwa mwakilishi pekee kutoka Tanzania.

Tuzo hizo ni za African Entertainment Awards USA zilizotolewa Oktoba 16 Jijini New York, Marekani na ya pili Star QT Awards zilizotolewa juzi nchini Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents