Burudani

Madam Rita, Salama na Master J walinifukuza BSS wakanambia “NATABASAMU” – Bwana Mjeshi (VIDEO)

Madam Rita, Salama na Master J walinifukuza BSS wakanambia "NATABASAMU" - Bwana Mjeshi (VIDEO)

Mchekeshaji kutoka kundi la Timamu BwanaMjeshi amefunguka A – Z kuhusu changamoto alizozipitia katika kazi yake ya Sanaa Mpaka kufikia hapa alipo sasa hivi.

Mjeshi amefunguka wakati anapiga stori na Bongo Five na kusema kuwa yeye alipitia changamoto nyingi sana hadi kufikia kusaidiana na mama yake mzazi kuuza Samaki mtaani,na ameahidi kuwa kuna siku atairudia biashara yake ya samaki.

Licha ya kuongelea changamoto hizo Mjeshi amefunguka juu ya mipango walionayo kama Timamu na kusema kuwa wanamipango mingi sana kwani wana Idea nyingi sana za kuzifanyia kazi, ingawa wanaendelea kupambana licha ya kutkuwa na pesa za kutosha za kusaidia kufanikiwa kwa kazi yao.

Mjeshi ameongeza kuwa wakati anaanza kazi ya Sanaa aliwahi kwenda kwenye mashindano ya Bongo Star Serch kwa lengo la kwenda kuonyesha kipaji chake lakini mwisho wa siku alifukuzwa na kuambiwa anaimba huku anatabasamu.

” Huwezi kuwalaumu Majaji wa BSS hao kwani nahisi muda haukufika maana wakati tuko kwenye tukio kuna mshiriki alikuwa anaimba sana hadi mimi damu zilisisimuka lakini alitoka analia licha ya kuimba kwake kote huko kwahiyo mi nikaona muda sio kama huyu anatoka analia mimi nani kwani mi si mtu tu”

Pia tulipiga stori na mchekeshaji mwenzake wa Timuma anayejulikana kama Mmasai na kusema kuwa yeye anakipaji kikubwa sana na anaweza kuigiza zaidi ya staili ya Umasai kwani anajua staili nyingi sana.

Kundi la Uchekeshaji la Timamu linaundwa na wachekeshaji Watatu ambao ni Bwana Mjeshi, Ebitoke pamoja na Mr Benfinchal au Masai licha ya kuwepo wengine hao ndio wachekeshaji wakubwa na wanaojulikana.

 

By Ally Juma.

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents