Burudani

Madee ajibu baada ya Chidi Benz kumuita Mnafiki

Msanii wa muziki Bongo kutoka Tip Top Connection, Madee amechukulia poa kauli ya Chidi Benzi aliyedai kuwa msanii huyo ni mnafiki.

Madee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Sikila’ aliyofanya na Tekno ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa hicho ni kitu kisichoweza kumuumiza kwa sababu siyo tusi.

“Chidi namuheshimu kama mdogo wangu kama rafiki yangu hatujawahi kutaniana. Ni kawaida sio tusi ambalo lingeweza kunifanya nichukie,” amesema Madee.

Kuhusu ujumbe aliandika katika mtandao wake wa twitter; ndio maana huwa sivuti sigara. Madee amekanusha ujumbe huo kumlenga Chidi Benz.

“Hilo ndio tatizo ambalo watu wengi wanashindwa kutafsiri ndio maana huwa napenda kujiita wino mweusi naandika kitu halafu kinakuweka wewe kwenye giza haujui, mpaka unitafute mimi nikueleweshe,” ameongeza.

Suala hilo lilifikia hapo baada ya Chidi Benz kudai kuwa amefanya kolabo na Tupac ambaye kwa sasa ni marehemu kitu kilicholeta mshangao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents