Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMahojiano

Lord Eyez akizungumzia maisha aliyopitia nyuma mpaka sasa

Kupitia Recap na Mando @el_mando_tz amepiga stori na gaidi la Rap kutoka Weusi, zamani Nako2nako Soldier LordEyez n akuongea mengi sana kuhusu maisha yake yote aliyowahi kupitia.

Mbali na hilo Lord Eyez ameachia EP yake mpya ya ABCD ambayo ina ngoma 5 na Intro ni ngoma namba moja na tayari ina video yake. Lord Eyez ambaye anajiita gaidi la rap pia amemzungumzia msanii wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya Kings Music Alikiba na kusema kuna ngoma mbili zinakuja moja ya Alikiba ft LordEyez na nyingine ya LordEyez ft Alikiba.

Lord Eyez ameongeza kuwa Alikiba sio msanii tu bali ni chombo cha muziki na kusema Tanzania imebarikiwa sana kuwa na msanii kama Alikiba.

Lord amezungumza mengi sana maisha waliyopita nyuma mpaka sasa, pia @lordeyesmweusi amesimulia namna mmoja wa wasanii katika kundi la Nako 2 Nako alivyopigwa kwenye pambano la ngomi.

Ameeleza kuwa mwenzao alipigwa kwani waliomba pambano na timu ya Boxing ya taifa baada ya kwenda Arusha.

Anasema baada ya kuona mwenzao anazidiwa yeye aliamua kuingilia kati kuamulia. pia amezungumzia walivyounda kundi la Nako 2 Nako na River Camp Soldiers na baadae kuzalisha Weusi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents