BurudaniMichezo

Makala: Asili ya aina za ushangiliaji za wanamichezo pindi wanapofunga

Tasnia ya muziki imekuwa bega kwa bega na michezo hata imekuwa ikiingiliana na wapenzi yaani wanaopenda michezo na muziki kwa wakati mmoja.Tumeona mara nyingi tu wanamuziki wakitunga mashairi yao wakijifananisha uwezo wao wa kimuziki na baadhi ya wanamichezo na hawajaishia tu katika mashairi yao bali hata wengi wao hutunga nyimbo zao na kuita nyimbo zao majina ya wanamichezo.

1974-Muhammad-Ali-George-Foreman-001315074
.
Mfano Mwana Hiphop wa nchini Marekani The Game mwaka 2012 kutoka katika albamu yake ya tano, aliachia wimbo unaokwenda kwa jina la ‘ ALI BOMAYE . ALI BOMAYE katika lugha ya kilingala ina maana ya ‘ ALI MUUE ‘ kwa Kiswahili na hii ilitokea katika pambano la kihistoria lililowahi kutokea duniani katika mchezo wa masumbwi baina ya MUHAMMAD ALI na GEORGE FOREMAN kati ardhi ya nchi ya Congo mnamo mwaka 1974 ambapo nashabiki waliokuwa wakiutazama mchezo huo walikuwa wakimpigia mayowe na kumuamuru MUHAMMAD ALI amuue GEORGE FOREMAN ‘ ALI BOMAYE (Ali Kill Him).

Na hata mwanamuziki kutoka Tanzania, Alikiba alitumia kionjo hicho katika wimbo wake wa ‘ Unconditionally Bae ‘ alioshirikiana na Sauti Sol Kutoka Kenya.

13768106_636604926489536_180045734_n
Khaligraph

Rapper kutoka Kenya, Khaligraph Jones, Septemba 2 mwaka 2015 alitoa wimbo JULIUS YEGO ‘ akifananisha uwezo wake mkubwa wa kurap kama mwanariadha huyo wa nchini Kenya mwenye mafanikio makubwa na akiwa ndo mwanariadha wa kwanza nchini humo kuweza kushinda medali ya dhahabu katika michezo ya Jumuiya ya Madola mnamo mwaka 2014.

Kama hiyo haitoshi, rapper G-Nako aliwahi kumshirisha Joh Makini kwenye wimbo wake alioupa jina ‘Juma Ikangaa.’ Juma Ikangaa aliyezaliwa Dodoma, alikuwa mkimbiaji wa mbio za marathon aliyeshinda mwaka 1989 kwenye mbio za New York City Marathon na kuweka rekodi ya kumaliza kwa 2:08:01. Ikangaa pia alishika nafasi ya pili kwenye Boston Marathon 1988-1990.

ikangaa_83

Uhusiano mzuri uliopo kati ya wasanii wa muziki na wana michezo ndio umepelekea hata baadhi ya wanamichezo kuweza kutumia aina za kucheza za wasanii hao kama aina ya ushangiliaji pindi wanafunga mabao.Hapa chini nitakuelezea aina ya ushangiliaji ya wanamichezo inayotokana na aina ya kucheza kutoka kwa wasanii wa muziki.

DAB

Dab ni aina ya kucheza ambapo mchezaji anashusha kichwa chini na kukilaza kwenye kiwiko huku mikono yake yote miwili akiwa ameinyoosha kuelekea juu katika uelekeo mmoja.Aina hii ya Uchezaji ina asili kutoka mji wa Atlanta nchini Marekani ambapo wana hiphop wengi mjini humo walikuwa wakiitumia na ilipata kuwa maarafu sana baada ya kikundi cha Wasanii wa Hiphop nchini Marekani ‘ MIGOS ‘ kuachia wimbo wao wa ‘ Look at my Dab ‘ na kupelekea baadhi ya wanamichezo kuitumia kama aina ya ushangiliaji

°CAM NEWTON

cam-newton-111615-getty-ftrjpg_109kzimizqgc71b3rse1zq1cd0

Ni mchezaji wa mpira wa kimarekani katika timu ya CAROLINA PANTHERS ambaye alikuwa kivutio kikubwa katika ligi kuu ya mpira wa kimarekani (NFL) .Mchezaji huyu wa nafasi ya robo ya kwanza ya nyuma alionekana kwa mara ya kwanza akisherehekea kwa aina ya Dab katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tennessee Titans mwaka 2015.Cam Newton alisema hata tumia tena aina ya ushangiliaji pindi mwaka 2016 utapoingia alipohijiwa na radio ya Charlotte.

°JEREMY HILL

CQpfmLdU8AAuosB

Jeremy Hill ambaye naye ni mmoja wa wanamichezo wa awali wa mpira wa kimarekani alionekana akitumia aina hiyo ya ushangiliaji alipofunga katika mchezo wa wiki ya kwanza baina ya Oakland Raiders Septemba 13 mwaka 2015.

°LEBRON JAMES

lebron-james-hits-the-dab-after

Mfalme huyu katika ligi kuu ya kikapu ya nchini Marekani alionekana kwa mara ya kwanza akicheza aina hii ya Dab baada ya kufunga katika mchezo wa awali kabla ya ligi kuanza (Pre Season) Octoba 5 2015.

°FRANK BEAMER

fra.0.0

Sio tu wachezaji wameonekana wakivutiwa na aina hii ya uchezaji bali hata Wakufunzi. Frank Beamer ni mkufunzi wa mpira alionekana akishangilia kwa dab.Kocha huyu wa zamani wa timu ya Virginia Tech baada ya kustaafu kukinoa kikosi hicho,Frank Beamer akabaki kuwa Mkufunzi klabuni hapo. Licha ya kuwa na miaka 70 lakini akaona hawezi kupitwa na ushangiliaji huu wa Dab.

°PAUL LABILE POGBA

2491972

Kiungo huyu wa Manchester United inawezekana ndio mwanamichezo ambaye anapenda aina hii ya ushangiliaji ya dab licha ya kuonekana mara kwa mara akishangilia kwa kucheza kwa aina ya dab vile vile pia alienda mbali zaidi hadi kuamua kujichora neno ‘ DAB ‘ katika upande wa kushoto katika kichwa chake ikiwa kama aina ya unyoaji wake.

Paul Labile Pogba aliitumia sana aina hii ya ushangiliaji alipokuwa na timu yake ya zamani ya Juventus huku alikuwa akipewa kampani na mchezaji mwenzake Paul Dyabala. Vilevile huwa anacheza aina hii ya Dab hadi akiwa katika timu yake ya taifa ya Ufaransa.Na ameonekana pia kuishawishi brand ya utengenezaji wa magemu ya video EA SPORTS kwani wameweka wazi kuwa aina hii ya ushangiliaji itapatikana katika gemu ya FIFA 17 pale ambapo Paul Labile Pogba akifunga ataonekana akishangilia kwa uchezaji wa DAB.

°JESSE LINGARD

maxresdefault

Winga huyu wa Machester United mwenye asili ya Uingereza ni moja ya wanamichezo wanayoipenda aina hii ya uchezaji ameonekana mara kwa mara akicheza mchezo huu pindi akifunga. Jesse Lingard amepata partner wakucheza naye katika club ya Manchester United baada ya kusajiliwa kwa Paul Pogba ambaye pia ni mpenzi wa uchezaji huo.

Alipost katika mtandao wake wa Instagram picha iliyounganishwa ya kwake na Paul Labile Pogba wakiwa wote wana DAB na wenye ujumbe wa kumkaribisha tena nyumbani.Jesse Lingard alishawahi kukiri kuwa amevutiwa na aina hii ya uchezaji baada ya kumuona Paul Pogba akishangilia kwa Dab pindi alipokuwa katika ligi ya nchini Italia SERIE A.

HOTLINE BLING DANCE

Aina hii ya Uchezaji inapatikana katika video ya wimbo wa rapper mwenye asili ya Canada Drake ‘ Hotline Bling ‘ uliotoka mwaka 2015 ambao ni wimbo wa kwanza kuachiwa kutoka katika albamu yake ya nne ‘ Views from the Six.

°ANTOINE GRIEZMANN

360DE81E00000578-0-image-m-16_1467967822080

Mshambuliaji huyu wa kifaransa alikuwa kivutio kikubwa katika michuano ya kimataifa ya Ulaya ya mwaka 2016 kwa aina yake hii ya uchezaji akiwa kama anapiga simu ‘ HOTLINE BLING DANCE ‘.Mshambuliaji huyu aliyetumbukiza nyavuni mara sita katika michuano hiyo alisema pia alikuwa akiitumia aina hii ya ushangiliaji hata pindi alipokuwepo katika Club yake ya Altetico Madrid ya nchini Hispania kwani alisema yeye ni shabiki mkubwa wa Drake na ametumia uchezaji huu kama kuonesha heshima kwa Drake.

Aidha pia Antoine Griezmann alisema alikuwa na furaha sana alipoifungia timu yake ya taifa Ufaransa goli la kwanza katika michuano hiyo dhidi ya Arbania na hadi ikampelekea asahau kushangilia kwa aina ya ‘ HOTLINE BLING ‘ na alisahau pia kucheza alipofunga goli la kusawazisha dhidi ya Ireland. Mshambuliaji huyu mwenye Magoli 22 katika ligi ya la liga msimu uliopita atakumbukwa pia kwa kuipeleka timu yake ya Ufaransa katika fainali ya michuano ya Euro baada ya kufunga mara mbili katika ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani.

HIT EM FOLKS

Ni aina ya uchezaji ambayo inahusisha kuinyoosha mikono ikiwa katika shepu ikisigana na wakati huo huo unaweza kuunyanyua aiza mguu wa kushoto au kulia.Mara nyingi aina za uchezaji katika ushangiliaji huwa zinaanzia katika nyimbo halafu wana michezo hukopi lakini imekuwa tofauti kidogo katika aina hii ya uchezaji uitwao ‘ HIT EM FOLKS ‘ kwani imeanzia michezoni ndipo wana muziki wakaichukua.

°ODELL BECKHAM Jr

falcons-giants_spaneru122-1

Mchezaji wa mpira wa miguu wa kimarekani wa timu ya New York Giants alionekana akishangilia katika ushindi wa 32-21 dhidi ya Washington Redskins katika uwanja MetLife. Kwa aina hii ya uchezaji huku ikiwa ni mara ya kwanza kuonekana kwa aina hii ya uchezaji katika ligi ya NFL .

Baada ya mchezo kumalizika Odell Beckham Jr,23 aliulizwa kuhusiana na aina hii ya ushangiliaji na alinukuliwa akisema ni aina ya uchezaji inayoitwa ‘ Hit Em Folks ‘ ni huwa wanaitumia sana katika mji wao wa Atlanta. Baada ya hapo aina hii ya uchezaji ikaanza kujizolea umaarufu na ndipo ikaingia katika muziki, Lil Uzi Vert ni mmoja ya wasanii wanaoitumia sana aina hii ya uchezaji katika nyimbo zake staa huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa anatamba na wimbo wake uitwao ‘ Camera ‘.

°JESSE LINGARD

1200

Winga huyu wa Manchester United alionekana kuja aina tofauti ya ushangiliaji baada alipofunga goli zuri ambalo alipokea mpira kutoka kwa Wayne Rooney na kukimbia umbali wa yardi 35 na kuwapiga chenga wachezaji wa Leicester city, Andy King na Danny DrinkWater na kumpita Wes Morgan ambaye alijaribu kumzuia na mwishowe akabaki na mlinda mlango Kasper Schmeichel na kuweza kumzidi ujanja baada ya kujaribu kuudaka mpira kwa kunyoosha mkono lakini juhudi zake ziligonga mwamba na Jesse Lingard aliweza kuingiza mpira wavuni na kisha kuanza kushangilia kwa aina ya ‘ Hit Em Folks ‘ katika mchezo huo wa ngao ya hisani, ambapo wengi walimzoea kushangilia kwa aina ya Dab lakini siku hiyo hali ilikuwa tofauti kidogo na kuongeza staili nyingine ya ushangiliaji katika mpira wa miguu ambapo aina hii ya uchezaji haijazoeleka katika mpira wa miguu.

WATCH ME (WHIP NAE NAE)

Watch Me ni wimbo wa kwanza wa Rapper Silento kutoka Atlanta nchini Marekani uliotoka tarehe 05/05/2015 ni wimbo uliofanya vizuri duniani kote hadi kuweza kushika nafasi ya 3 katika chati za muziki za billboard za nyimbo bora 100.
Kufanya vizuri kwa huu wimbo uliambatana na aina yake ya uchezaji ya utikisaji miguu na kuutupa mkono moja mbele na mguu ikiwa inaenda tofauti yaani kama ukiutupa mkono wa kulia unaambatana na mguu wa kushoto.

°MEMPHIS DEPAY

maxresdefault (1)

Katika mchezo wa kufuzu wa ligi ya mabingwa ulaya baina ya Manchester United na Club Brugge uliomalizika kwa Manchester United kushinda 2-1.Memphis Depay aliweza kuifungia club yake ya Manchester United mabao yote mawili.Baada ya kuifungia klabu yake goli la pili. Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Uholanzi alishangalia ushindi huo kwa kucheza aina hii ya uchezaji ‘ Watch me Whip Nae Nae ‘.

Imeandaliwa na
FARAJI FOWZ ZEGGESON

Instagram @xfowz
Twitter @Fowzwheezy
[email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents