Burudani

Makala: Damian Soul ‘aliwateka’ wakali sita wa Hip Hop Bongo

Damian Soul ni miongoni mwa wasanii wachache wanaofanya vizuri Bongo katika mahadhi ya muziki wa Soul unaokaribia kufanana na RnB.  Damian ana aina yake ya muziki na vile vile ana sauti yake ya kipekee zaidi.

Damian Soul jukwaani na Grace Matata

Ndiyo, sauti yake ni ya kipekee zaidi. Wakati Damian Soul anatoka na ngoma yake ya ‘Hakuna Matata’, watu wengi hawakuamini kama ‘mtoto wa kiume’ anaweza kuwa na sauti kama ile, mimi mwenyewe nilikuwa mmoja wapo. Tuachane na hilo.

Kwa sasa jina lake ni kubwa, kila shabiki wa Bongo Fleva anamjua Damian Soul ni nani, na uwezo wake ni upi kwenye kuimba kwakuwa ameshatoa nyimbo nyingi kama vile Ni Penzi, Dua la Kuku, Baraka na Tudumishe, na zimefanya vizuri kwa kiasi kikubwa.

Msanii AY alipoulizwa na kipindi cha Mkasi kuhusu wasanii anaowakubali kutoka kwenye Bongo Fleva, alimtaja Vanessa Mdee na Damian Soul, hii inaonyesha ni kwa namna gani anavyokubalika, na hasa kwa upande wa wakali wa muziki wa Hip Hop.

Kwa kulitambua hilo leo ninakuletea orodha ya wakali sita wa Hip Hop kutoka Bongo waliomshirikisha Damian Soul kwenye ngoma zao ili kuzinogesha kwenye upande wa kiitikio (chorus).

  1. Lord Eyes

Tunaweza kusema huyu ndiye msanii wa kwanza kugundua Damian Soul ‘anafiti’ katika ngoma za Hip Hop, Lord Eyes alimpa shavu kwenye ngoma yake itwayo ‘Mapito’.

Baadhi ya watu walihoji kuhusu uwezo wa Damian Soul, ‘inakuwaje msanii mchanga kupewa nafasi kama ile tena na msanii mkubwa’, ili bahati nzuri kadiri siku zilivyokuwa zikisongea ndivyo alivyodhihirisha kuwa alistahili kupewa nafasi hiyo.

Ikumbukwe ngoma ya Mapito Lord Eyes aliiandika mara baada ya kupitia misukosuko kwa kile kilichodaiwa kuwa aliiba vifaa vya gari vya msanii mwenzake, yaani OmmyDimpoz, hivyo ngoma hiyo ilitumika kama sehemu ya kujibu tuhuma hizo.

  1. Zaiidi

Huyu ni msanii wa Hip Hop anayewakilisha vema TamaduniMuziki kwa sasa, achilia mbali uwezo wake wa kuchana na kuandika misitari, pia Zaiidi amekuwa na uwezo wa kurudia nyimbo (cover) za wasanii wengine.

Nyimbo hizo mara nyingi huwa za wasanii wa nje lakini yeye huzirudia kwa lugha ya kiswahili. Anachofanya yeye ni kuchukua ‘melody’ na ‘beat’ tu, kisha anatumbukiza mashairi yake, alishafanya hivyo katika ngoma ya J Cole ‘Who Dat’ na ule ya FettyWap ‘Trap Queen’ ila yeye akaipa jina la Madebe.

Zaiidi alimshirikisha Damian Soul kwenye wimbo uliyokwenda kwa jina la ‘Mistai Yakoambao alikuwa anaelezea masuala ya mahusiano ya kimapenzi.

  1. Young Killer

Baada ya kutoka na ngoma ya Dear Gambe aliyompashavu Belle 9 ambayo iliyomtambulisha kwenye muziki wa Bongo Fleva, kisha Miss Super Star aliyofanya na Bright pamoja na Nemo, Damian Soul nae akachukua nafasi yake.

Young Killer alimpashavu Damian kwenye wimbo wake ‘My Power’ uliyofanywa na maprodyuza wawili ambao ni Mona Gangster na Rash Don. Kama mpangilio wa Young Killer toka mwanzo ulilenga wakali wanaojua kucheza na sauti zao, basi alilenga penyewe.

  1. Songa

Anayewakilisha vema Tamaduni Muziki, kwa sasa anatamba na ngoma yake ijulikanayo kama ‘Mwendo Tu’ aliyompashavu Jay Moe.

Hivi majuzi ameshinda tuzo zinazotolewa na tovuti ya mdundo.com, Songa ameshinda kama msanii bora ya Hip Hop kutoka na nyimbo zake kupakuliwa (downloads) zaidi katika mtandao huo.

Songa nae hakuwa nyuma kumpa shavu Damian Soul, walifanya kazi pamoja na kutoa wimbo uitwao ‘I Know You Now’ .kwa bahati mbaya wimbo huu haukutoka katika vyombo vya habari, hivyo huenda wanao ufahamu ni wachache.

  1. One the Incredible

Huyu ni mkali wa hip hop mwenye albam mbili mkononi hadi sasa, ya kwanza ni ‘Soga zaMzawa’ iliyotoka mwaka 2012 na ya pili ni ‘Rap’ iliyotoka mwaka 2015.

Pia One the Incredible hakuwa mbali kuinasa sauti ya Damian Soul, alimpa nafasi kwenye ngoma inayokwenda kwa jina la ‘Yeye’ iliyopikwa na prodyuza Dunga.

  1. Mansu-Li

Amedumu kwa muda kwenye muziki wa Bongo Fleva, ana albam moja mkononi inayokwenda kwa jina la ‘Kina Kirefu’ aliyotoka kati ya mwaka 2012/2013 ambayo ilijumuisha ngoma zake nyingi tangu anze muziki.

Na yeye alitambua uwezo wa Damian Soul na kuamua kufanya nae kazi, wimbo ulitambulika kama ‘Kila Sababuiliyofanyika kwenye studio zaTongweRecods.

Chukua na hii pia

Stori zilizopo nyuma ya pazia zinasema ngoma ya Nikki Mbishi ‘Sihusiki Nao’ aliyompashavu Walter Chilambo, awali ilipangwa Damian Soul ndiye angeimba kiitio (chorus) chake, lakini hilo likashindikana kutokana na sababu fulani.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents