Michezo

Manara: Serikali ihakiki upya leseni za udereva

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kutokana na matukio ya ajali yanayoendelea kutokea hapa nchini, kuna haja Serikali kuhakiki upya leseni za udereva.

Haji Manara

Kupitia mtandao wa kijamii wa instagram, Manara amesema “Ni kweli ajali hupangwa na Mungu lakini nyingine zinaepukika, kuna haja Serikali kuhakiki upya leseni za udereva kama walivyohakiki vyeti vya magumashi.

Katika hatua nyingine Manara alitoa salamu za pole kwa watu wote waliofikwa na msimba wa wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent mkoani Arusha.

“Hakika ni Janga kubwa, ni pigo kuu, tunapaswa kama Taifa tuumie wote kwa msiba huu mzito, poleni wazazi na walimu wote nchini, Simba SC inaungana nanyi katika kadhia hii nzito kabisa kuwahi kutokea katakea ajali za barabarani hapa kwetu Tanzania,” ameandika Manara.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents