Michezo

Himid Mao kuanza mtihani wa majaribio kesho

Kiungo wa klabu ya Azam FC, Himid Mao Kesho Jumanne anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa majaribio akiwa na kikosi cha akiba cha timu ya Randers FC, inayoshiriki ligi kuu ya nchini Denmark.
Image result for himid mao
Himid Mao akiwa Denmark kwenye uwanja wa Klabu ya Randers FC
Himid Mao aliondoka nchini wiki iliyopita kwenda Denmark kwa ajili ya majaribio na Klabu ya Randers FC inayoshiriki ligi kuu ya Denmark atajifua kesho kwenye mchezo wake wa kwanza wa majaribio.
Taarifa kutoka kwenye mtandao wa klabu hiyo zimesema kuwa kiungo huyo atakuwepo katika mechi  hiyo ya kikosi cha akiba cha timu hiyo kabla ya kuamua kumsajili.
“Himid Mao ni mchezaji wetu hivyo nae atakuwa sehemu ya klabu yetu katika mechi ya wachezaji wa akiba dhidi ya AC Horsens “Umeandika mtandao wa klabu ya Randers FC.
By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents