Michezo

Diego Maradona alamba shavu nono uarabuni

Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Barcelona Muargentina, Diego Maradona ’56’ baada ya kibarua chake cha kuinoa klabu ya Al Wasl kuota nyasi, hatimaye amepata klabu ya kuitumikia.

Diego Maradona amepata shavu la kuinoa klabu ya Al-Fujairah FC, ya Uarabuni  kama kocha mkuu hii ikiwa ni kazi yake ya kwanza kwa miaka mitano toka afukuzwe  na klabu ya Al Wasl mnamo July 2012.

Klabu ya Al-Fujairah kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii waliweka picha ya Maradona na kuthibitisha usajili huo.

Diego Maradona kwenye dili hilo ataingiza kiasi cha Dola 800,000 za Kimarekani na ameahidiwa kuongezewa mkwanja endapo klabu hiyo itachukua kombe lolote kwa msimu huu.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents