Bongo5 Makala

Makala: RC Makonda anagusa maisha ya wengi

Matokeo ya sensa ya mwaka  2012 yanaonyesha Mkoa wa Dar es salaam una watu wengi kuliko mkoa mwingine wowote Tanzania Bara, ambapo una jumla ya watu milioni 4.36.

Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwezi Agosti mwaka 2012, Tanzania ina jumla ya idadi ya watu milioni 44,929,002 . Matokeo hayo yalionyesha ongezeko la idadi ya watu nchini lililofikia watu milioni 33,000,000 ikilinganishwa na sensa iliyofanyika baada  ya uhuru ambapo ilionyesha Tanzania ina watu milioni 12,313,054.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Twaweza  unaeleza kuwa wananchi 6 kati ya 10 ni sawa asilimia 61, ambao  hufika katika vituo vya afya vya serikali pale mtu anapougua au kuumia. Hii inafanana na utafiti uliofanywa mwaka 2016 ambao ulionesha ongezeko kutoka mwaka 2014 na 2015, ambapo chini ya nusu ya wananchi (45-47%) walitumia vituo vya afya vya serikali.

Kwanini RC Makonda

“Aliyeshiba hamjui mwenye njaa,” lakini kuna walioshiba wanawakumbuka wenye njaa pia. Hili nimeliona kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Hivi karibuni nilikuwa nikitazama kwa jicho la tatu utendaji kazi wa kiongozi huyo kwa kufanya mambo mengi zaidi ya kijamii lakini katika mambo yote nilipenda suala la kupima afya bure kwa wakazi wa jiji lake lililofanyika kwa siku 5 kuanzia tarehe 7 hadi 11.

Kila mtu anajua kuwa afya ni muhimu kwa kila mtu kwasababu usipokuwa na afya huwezi kufanya chochote katika dunia hii, ni kweli kwamba hakuna mkamilifu chini ya jua ila kunapokuwa na jambo jema limefanywa na kiongozi yoyote la kugusa jamii ni lazima tuliseme na tulisifie na si kwamba viongozi wengine hawafanyi mambo mazuri lahasha! mimi nimeona nizungumzie kidogo utendaji kazi wa Mkuu wa mkoa wa Dar.

RC Makonda kupitia vyombo vya habari alitangaza suala la wakati wa jiji la Dar kupima afya bure, ambapo walikuwa ni wengi na mimi nilishuhudia uwepo wa watu wengi katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambapo hakuna mtu aliyetegemea kujaa kwa watu kiasi kile ambapo kuliwekwa ulinzi wa kutosha wa polisi .

Uanzaji wa matibabu ulikuaje:
Huduma hiyo ilipangwa Jumatano hadi Jumapili ambapo ulikuwa unachukua namba kwa mtiririko huo ili iwe haki sawa kwa wote waliokuwepo eneo hilo waliokuwa wakisubiri matibabu mbalimbali ambapo huduma mbalimbali zilikuwa zikitolewa.

Madaktari:
Madaktari wa hospitali mbalimbali walijitokeza kujitolea kwaajili ya kuwahudumia wananchi kupitia mkuu wa mkoa huyo, ambapo baadhi ya hospitali ni Aghakhan, TMJ, Muhimbili na nyinginezo.

Utoaji huduma kwa madaktari:
Madaktari walikuwa ni wakarimu wakiwa hudumia wa gonjwa kwa upendo ni jambo ambalo hata mimi kwa macho yangu nililishudia, wagonjwa walikuwa wanapimwa uzito kwanza , pressure, kama una magonjwa ya moyo na magonjwa mengine mbalimbali makubwa kama figo,kisukari, saratani, macho, homa ya ini .

Wananchi walilizungumziaje tukio la Makonda kutoa huduma ya kupima afya bure:
Wananchi waliokuwepo katika eneo hilo na baadhi ya waliokuwepo mitaani waliposikia zoezi hilo walifurahi sana na kushukuru huku wakisema uwezo wa kupima magonjwa hayo hawana kwasababu gharama zake ni kubwa, ndio maana waliposikia fursa hiyo wakaona ni vyema wajumuike katika zoezi hilo la kupima afya bure.

Baada ya kupima ikawaje:
Mkuu wa Mkoa huyo baada ya kupima afya alisema wakigundulika na tatizo watapewa vibali vya kupelekwa katika hospitali zilizojitolea kwa kuongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Dk Grace Maghembe.

Hali ya eneo lile ilikuaje:
Kama tunavyoelewa jiji la Dar lina kuwa na joto mara nyingi kuliwekwa na baadhi ya Mantente ambapo Mkuu wa mkoa huyo aliagiza kuongezwa mengine kwaajili ya kuzuia jua lilikowepo katika eneo lile pamoja na kuwanunulia maji ili kupooza koo kidogo wakati wana subiri huduma.

Hali ya ukawaida:
RC Makonda alikuwa na uwezo wa kutofanya zoezi hilo kwasababu kama kiongozi alikuwa na uwezo wa kutibu afya yake yeye kama yeye lakini akaona mbali kwamba wapo watu ambao wanaumwa na hawana uwezo wa kwenda hospitali kupata matibabu .

Amefanya mengi kwa nafasi yake aliyonayo ila kwa hili la afya aliona mbali na si mara ya kwanza kufanya zoezi hili kwa wakazi wa mkoa wake. Kwahiyo natoa pongezi kwake na Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya zoezi hili la watu kupima afya bure kwa mkoa wa Dar japo kuwa si wakazi wa Dar tu walikuwepo walikuwepo baadhi ya watu wa mikoani.

Mkuu wa Mkoa huyo siku ya kwanza alitoa shukrani kwa waandishi wa habari kwa kupaza sauti kwa wananchi kuwahamasisha wananchi kuhudhuria katika zoezi la upimaji wa afya bure na jeshi la polisi kwa ulinzi .

Historia ya jiji la Dar es salaam:

Kwa mujibu wa tovuti ya mkoa wa Dar es salaam , Jiji la Dar es Salaam lilianza kama Kijiji kidogo cha wavuvi kilichojulikana kama Mzizima. Kijiji hiki kilianzishwa na Wabalawa ambao walichanganyika na Wazaramo kuelekea kwenye maeneo ya Bara la Afrika Mashariki na ambazo zilijulikana kama ‘Caravan Routes’. Ujenzi wa Makao ya Sultani pamoja na bandari ulianza rasmi mwaka 1865 katika eneo la kijiji cha Mzizima. Ujenzi huo ulikamilika mwaka 1866 na Sultani Majid bin Said kuhamia Dar es Salaam mwaka huo.

Mara baada ya Sultani Majid bin Said kuhamia Dar es Salaam mji ulianza kupanuka na uchumi wake kukua kwa kasi kubwa japo kwa kipindi kifupi ambapo Sultani Majid bin Said alifariki mwaka 1870. Kifo cha Sultani huyo kilisababisha kudidimia kwa maendeleo ya mji wa Dar es Salaam. Hali hiyo ilianza tena kubadilika mwaka 1884 kufuatia kuanzishwa kwa koloni la Wajerumani la Afrika Mashariki.

Mwaka 1891 Serikali ya kikoloni ya Kijerumani iliamua kuhamisha makao makuu ya utawala wake katika Afrika Mashariki kutoka Bagamoyo na kuyaweka Dar es Salaam. Hata hivyo, baada ya Wajerumani kushindwa na Waingereza katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mwaka 1916, Mji wa Dar es Salaam uliendelea kuwa makao makuu ya utawala wa koloni la Waingereza nchini Tanganyika hadi ilipojipatia uhuru wake mwaka 1961. Dar es Salaam iliendelea kuwa makao makuu ya Tanganyika huru na hatimaye kuwa makao makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi mwaka 1972 wakati Serikali ilipoamua kuhamishia makao yake makuu mjini Dodoma. Jiji la Dar es Salaam liliendelea kubaki kuwa maarufu kwa kuwa Jiji kuu na kitovu cha biashara nchini Tanzania.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents