Bongo5 MakalaBurudani

MAKALA: Vijana 30 wenye ushawishi zaidi kwa mwaka 2017 nchini Tanzania

Ukiwa mwaka 2017 unaelekea ukingoni ni vyema tukaangalia orodha ya vijana 30 Wakitanzania ambao wamefanya vizuri kupitia kazi zao wanazofanya.

Orodha ya majina haya yanaangalia vijana waliofanya vizuri kwenye Ujasiriamali, Sanaa na Michezo. Ambapo kuna majina ya vijana 30 wenye ushawishi zaidi nchini Tanzania na orodha hii ni kwa mujibu wa Mtandao wa bongo5.com .

1-DIAMOND PLATNUMZ.

Mwaka 2017 umekuwa mwaka mzuri na wamafanikio zaidi kwa Diamond Platnumz kwani licha ya kufanya vizuri kwenye muziki. Diamond amefanikiwa kuanzisha biashara ya Karanga (Diamond Karanga),  Manukato (Chibu Perfume), na mtandao wake wa kuuza nyimbo mtandaoni (wasafi.com) kitu ambacho kimemuongezea ushawishi maradufu kwenye ujasiriamali.

Diamond pia kupitia muziki ameshinda tuzo kibao zikiwemo za AELA, Hipipo, Too Exclusive na tuzo ya heshima aliyopatiwa na lebo ya Universal Music Group (UMG) baada ya kufikisha mauzo ya Platnumz 6.

Kwa mwaka 2017, Diamond amefanikiwa pia kupata dili kadhaa za matangazo yakiwemo matangazo ya Vodacom na maduka ya Danube.

2-MILLARD AYO.

Kwa miaka miwili mfululizo Millard Ayo amekuwa na mafanikio makubwa kwenye kazi yake ya Utangazaji na Uandishi wa Habari kupitia Blog yake ya (millardayo.com) na Channel yake ya Tv mtandaoni (AyoTV) kitu ambacho kimewafanya vijana wengi kuvutiwa na kazi zake.

Mbali na kazi yake ya uandishi wa habari na utangazaji pia Millard Ayo amepata dili za matangazo na mtandao wa simu za mikononi wa Vodacom na maduka ya Danube.

3-ALIKIBA.

Kwa mwaka 2017, Alikiba kupitia muziki amefanikiwa kufungua lebo yake ya muziki ya  King’s Music, Kushiriki kwenye msimu wa tano wa Coke Studio Africa na kushinda tuzo kibao.

Alikiba kwa mwaka 2017, ameshinda tuzo za AFRIMMA, Hipipo, AEAUSA na kutunukiwa tuzo ya heshima na lebo yake ya Sony Music Africa kwa kufikisha views milioni 5 kwenye mtandao wa YouTube kupitia wimbo wake wa AJE.

Pia mwaka 2017, Rockstar4000 walimtangaza Alikiba kuwa ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya Rockstar4000 Music Entertainment Co & Rockstar Television.

Utakumbuka awali Alikiba alikuwa msanii wa kawaida chini ya RockStar4000 pamoja na Barakah The Prince ambaye kwa sasa hayupo tena katika label hiyo. Hivyo ni vitu ambavyo vimemuongezea ushawishi kwa vijana kwa mwaka 2017.

4-IDRIS SULTAN.

Muigizaji na Mchekeshaji Idriss Sultan kwa mwaka 2017 amefanikiwa kuingia kwenye ujasiriamali kwa kuanzisha biashara ya viatu ya (SultanXForemen) na kupata dili kibao za matangazo yakiwemo SportPesa, na matangazo kibao ya bidhaa za Ngano na viberiti kutoka Kampuni ya MeTL.

Kupitia kazi yake ya Uigizaji Idris amefanikiwa kuchukua tuzo kibao zikiwemo tuzo za ASFA na kufanikiwa kupata dili la kuigiza kwenye filamu ya ‘The Blue Mauritius’ nchini Marekani. Filamu hiyo itaanza kutengenezwa mwezi Machi mwakani ambapo kazi hiyo inasimamiwa na kampuni mbili za utengenezaji wa filamu kutoka Marekani ikiwemo D Street Pictures na Benoraya Pictures.

Pia Idris Sultan mwaka 2017, amefanikiwa kucheza kwenye filamu ya Kiumeni, Filamu ambayo ni moja ya filamu zilizofanya vizuri Tanzania ikiongozwa na Ernest Napoleon.

5-JOKATE MWEGELO.

Kwa mwaka 2017, Muigizaji na Mjasiriamali, Jokate Mwegelo hajafanya vitu vingi kwenye tasnia hiyo lakini amefanya vizuri kwenye jamii kwa kutoa misaada kwa baadhi ya shule za sekondari.

Jokate kwa mwaka huu ameonesha nia ya kujituma kwenye michezo upande ambao watu wengi hawakujua kama anaupendo na mchezo wa kikapu, ambapo amejenga uwanja wa mpira wa kikapu katika shule ya sekondari Jangwani na kuteuliwa kuwa balozi wa mchezo huo Tanzania.

Jokate mwaka 2017, ametajwa na jarida maarufu duniani la Forbes kama vijana walio chini ya miaka 30 waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali pia ameshinda tuzo ya malkia wa nguvu iliyoandaliwa na Clouds Media Group.

Kwa upande mwingine Jokate amefanikiwa kupata matangazo mbalimbali yakiwemo ya SportPesa na ya Juice ya Shake & Sippy.

6-VANESSA MDEE.

Mwaka wa 2017, umekuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwa msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ambaye kupitia muziki amepata  dili la kuigiza kwenye series za MTV Shuga. Na ni moja ya wasanii wa kike waliofanya kolabo nyingi za kimataifa na wasanii wa nje.

Vanessa Mdee

Vanessa Mdee pia kwa mwaka 2017 ameufunga kwa kusaini dili kubwa na kampuni ya kimataifa inayojihusisha na kusimamia kazi za wasanii ya Universal Music Group.

7-JOTI.

Kwa upande wa uchekeshaji, Joti kwa mwaka 2017 ameuvuruga kwa kiasi kikubwa japokuwa kazi zake zote amezifanya akiwa na Kampuni yake ya Joti Entertainment.

Joti

Amejitahidi kuonesha uwezo wake nje ya kazi za Orijino Komedi kama ilivyokuwa imezoeleka kwa miaka ya hivi karibuni.

Mbali na kazi yake ya uchekeshaji Joti amefanikiwa kufanya matangazo na Makampuni lukuki yakiwemo DSTv, tiGO, Uber Tanzania, BIKO, na bidhaa za  Kung-FU Energy na Chips Snacks.

Ni ukweli usiopingika kuwa Joti ndio msanii pekee aliyefanya matangazo mengi kwa mwaka 2017.

8-FARAJA NYALANDU.

Miss Tanzania mwaka 2004 na Mjasiriamali, Faraja Nyalandu kwa mwaka 2017 ameendelea kujikita zaidi katika kusaidia jamii kwenye sekta ya elimu kupitia mtandao wake wa Shule Direct.

Faraja Nyalandu

Mbali na mchango wake mkubwa aliyouonesha kwenye elimu pia amefanikiwa kupata matangazo na Benki ya NMB ambapo amekuwa balozi wa Benki hiyo yenye wateja wengi nchini Tanzania.

9-MBWANA SAMATTA.

Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars na klabu ya KRC Genk kwa miaka miwili mfululizo amefanya vizuri sana kwenye soka sio tu kwenye timu ya taifa bali hata kwenye klabu yake.

Mbwana Samatta

Samatta mpaka sasa yupo kwenye 10 ya wafungaji wenye magoli mengi ya Ligi Kuu Ubelgiji, Pia alitajwa kwenye tuzo kubwa barani Afrika za mchezaji bora wa mwaka.

Kutokana na ushawishi wake kwenye soka Samatta amefanikiwa kupata matangazo na Benki ya DTB Plc.

10-MAULID KITENGE.

Sio jina geni kwa masikio ya wadau wa soka hapa nchini Tanzania kwani sauti yake karibia kila siku za wiki na hata wikiendi ni lazima uisikie.

Maulid Kitenge

Maulid Kitenge kwa mwaka 2017, kupitia kipindi cha Sports HeadQuarter (Sports HQ) amekifanya kipindi hicho kipate jina zaidi kwa mwaka 2017.

Licha ya kwamba kuna watangazaji na wachambuzi wa soka wengi  kwenye kipindi hicho lakini namna ya uwasilishaji wake pindi anapokuwa hewani kwa mwaka huu kumemuongezea ushawishi zaidi na kukifanya kipindi cha Sports HQ kuwa moja ya vipindi bora vya michezo kwa mwaka 2017.

Kitenge mbali na kazi yake na E-FM amefanikiwa pia kupata dili na SuperSport kutangaza mechi za EPL kwa lugha ya kiswahili na amefanya pia matangazo na kampuni ya BIKO.

11-RAYVANNY.

Rayvanny mwaka 2017, kupitia muziki ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kushinda tuzo ya BET nchini Tanzania.

Rayvanny

Amefanikiwa pia kurekodi vipindi vya Coke Studio Africa season 5 ambapo aliweza kutumbuiza na msanii mkubwa kutoka Marekani, Jason Derulo.

12-FELIX SIMBU.

Huyu ni Mwanariadha wa mbio ndefu ambaye kwa mwaka 2017, ameiweka Tanzania kwenye ramani ya michezo hiyo kwa kutwaa medali kadha wa kadha.

Mshindi wa Medali ya Shaba katika mbio za dunia za London Marathon, Alphonce Felix Simbu (kulia)

Alphonce Simbu, amefanikiwa kushinda medali ya Kwanza ya Dhahabu kwa Tanzania katika mbio ndefu za Mumbai Marathon za mwaka huu akiwapiku Mkenya Joshua Kipkorir pamoja na wakimbiaji wengine wazoefu kutoka mabara mbalimbali.

Na kikubwa zaidi Simbu kwa mwaka huu amefanikiwa kushika nafasi ya tano bora kwenye mbio maarufu duniani za London Marathon na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania akitwaa medali ya shaba.

Ushindi wa Simbu umerudisha ari kwa vijana kwenye mchezo wa riadha kwa kiasi kikubwa na amefanikiwa pia kupata matangazo na baadhi ya makampuni kama DSTv .

13-FLAVIANA MATATA

Mwanamitindo Flaviana Matata kwa mwaka 2017 amefanikiwa kuzindua bidhaa zake za rangi ya kucha aina ya Lavy.

Flaviana Matata

Mbali na kazi yake ya mitindo Mrembo Flaviana kupitia Foundation yake ya (Flaviana Matata Foundation) amefanikiwa pia kusaidia wanafunzi wa kike kwenye mashule mbalimbali hapa nchini.

14-JACQUELINE MENGI.

Licha ya kuwa na uwezo mkubwa kwenye kuimba lakini kwa miaka ya hivi karibuni, Jacqueline Mengi amejikita kwenye ujasiriamali na ukweli ni kwamba kwa mwaka 2017 ameonekana kufanya vizuri zaidi.

Jacqueline Mengi

Kwa mwaka 2017, Jackline amefanikiwa kibiashara kupitia maduka yake ya samani ya Molocaho Amorette.

Mbali na Ujasiriamali pia kupitia Foundation ya Dr Ntuyabaliwe kama Mkurugenzi Mtendaji amesaidia kujenga maktaba kwa shule nyingi za Sekondari na Msingi jijini Dar es salaam.

15-HERIETH PAUL.

Mwanamitindo Herieth Paul ambaye kazi zake anafanyia nchini Marekani kwa mwaka 2017, kupitia tasnia hiyo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa ku-cover majarida makubwa ya fasheni duniani.

Ukiachana na matangazo ya bidhaa za vipodozi, Herieth amefanikiwa kuonekana kwenye maonesho maarufu ya fasheni duniani ya Victoria Secret nchini Ufaransa.

16-NANCY SUMARI.

Moja kati ya wanawake waliofanya vizuri kwenye ujasiriamali (Social Entrepreneurship) kwa mwaka 2017 ni Nancy Sumari. Mkurugenzi huyo wa Bongo5 Media Group kupitia taasisi ya The Neghesti Sumari Foundation chini ya Jenga Hub ameweza kushinda shindano la Tigo Digital Change Makers.

Nancy Sumari

Nje ya kazi zake za ujasiriamali, pia amefanya matangazo na kampuni ya Multichoice kupitia bidhaa yao ya DSTv.

17- ERNEST NAPOLEON.

Muigizaji na Muaandaaji wa filamu, Ernest  Napoleon mwaka 2017 amefanikiwa kuachia filamu yake ya Kiumeni ambayo ni moja kati ya filamu zilizofanya vizuri kwa mwaka huu.

Ernest  Napoleon

Pia amepata dili kubwa la kucheza filamu ya Hollywood ya ‘The Blue Mauritius’ ambayo inatarajiwa kutoka mwakani.

18-REBECA GYUMI.

Huyu ni Mwanaharakati wa kwanza Tanzania kupaza sauti ya kupinga ndoa za utotoni, Rebeca Gyumi mwaka jana alishinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Malengo ya dunia katika kipengele cha mabadiliko ya kijamii.

Rebeca Gyumi

Ni muanzilishi wa Shirika binafsi la Msichana Initiative ambalo linafanya kazi ya kuwanyanyua watoto wa kike kielimu.

19-MARIA SARUNGI TSEHAI.

Huyu ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communication na ni moja ya Wajasiriamali ambao wamefanya vizuri kwa mwaka 2017, Amehusika kuratibu mashindano ya Miss Universe 2017 na amehudhuria pia kwenye mikutano mikubwa ya kimataifa.

Maria pia ni Muanzilishi wa Kwanza TV na mwishoni mwa mwaka huu ameanzisha kipindi cha ‘Njoo Tuongee’ kinachoruka kupitia Star TV ambacho kinajadili masuala mbalimbali ya kijamii.

20-CAROL NDOSI.

Kama huwa unasikia matamasha ya Nyoma Choma ambayo hufanyika mikoa mbalimbali basi nyuma ya  Tamasha hilo yupo Mjasiriamali, Carol Ndosi.

Ingawaje ni nguli wa masuala ya Media lakini kwa mwaka 2017 amejikita zaidi kwenye masuala ya Ujasiriamali.

Tamasha la Nyama Choma limekuwa likiwavuta maelfu ya vijana na kwa mwaka 2017, ameweza kuwavutia wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kiasi kikubwa sana, Ikiwemo kuwashika mkono katika Matamasha hayo, kutoa elimu ya Ujasiriamali mtandaoni kupitia majukwaa tofauti tofauti.

21-LIL OMMY (OMAR TAMBWE).

Moja kati ya Watangazaji wa Radio hususani kwenye vipindi vya Burudani kwa mwaka 2017, Lil Ommy amefanya vizuri sana kupitia kipindi chake cha Playlist kinachoruka Times FM.

Lil Ommy

Lil Ommy sio tu amewavutia wasikilizaji wake bali hata mashabiki wa muziki ambao mara wamekuwa wakiwachana watangazaji wenye upendeleo kwa baadhi ya wasanii.

Uulizaji wa kipekee wa maswali umemfanya kipindi chake cha Playlist kuwa moja ya vipindi bora vya radio kwa mwaka 2017.

Lil Ommy pia kwa mwaka 2017, amefanikiwa kufanya matangazo na Kampuni ya TECNO, Serengeti Premium Lite, Coke Studio Afrika na Jumia Food.

Pia ametajwa na Kituo cha runinga cha Trace TV tawi la Kenya kama mtangazaji bora anayesapoti kazi za wasanii kwa mwaka 2017.

Ametajwa na gazeti la Bingwa kama mtangazaji bora wa mwaka 2017 na alipata mualiko maalumu kuhudhuria tuzo za AFRIMA nchini Nigeria mwezi Septemba, 2017.

22-SIMON MSUVA.

Simon Msuva amekuwa na mwaka mzuri kwenye timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) pia hata kwenye klabu yake mpya ya Difaa El Jadid aliyosajiliwa akitokea Yanga.

Simon Msuva

Simon Msuva msimu wa 2016/2017 ametwaa tuzo ya mfungaji bora wa msimu akiwa na magoli 14 aliyoifungia klabu yake ya Yanga.

Mbali na ushindi huo wa Tuzo, pia Msuva mwezi mmoja baada ya kujiunga na klabu ya Difdaa El Jadid alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti, 2017.

23-ASLAY.

Baada ta kutangazwa kuwa kundi la Yamoto Band limesambaratika na kila msanii kufanya kazi kivyake, mapema mwezi wa April mwaka 2017, ndio ulikuwa mwanzo wa Aslay kuanza kuonesha uwezo wake binafsi kama Solo Artist, ambapo alifanikiwa kutoa Hit zaidi ya 10 mpaka kufikia mwezi Desemba 2017.

Aslay

Aslay kwa uwingi huo wa ngoma kali, hakuna ubishi kuwa kumemrudishia jina maradufu kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kitu ambacho kimemfanya asikilizwe zaidi na kupata show kibao kwa mwaka 2017.

Kupitia muziki Aslay ameshinda tuzo za AFRIMA nchini Nigeria na amefanikiwa pia kutajwa kwenye tuzo kubwa nchini humo za Soundcity MVP.

24-DAVID OMARY (Dj D-OMMY).

The International DJ kama mwenyewe anavyojiita ni moja ya Ma Dj bora Afrika kwa mwaka 2017, ingawaje hajashinda tuzo hata moja lakini mwaka 2017 amekuwa nominated kwenye tuzo kibao za kimataifa zikiwemo AFRIMA, AEAUSA na nyinginezo.

DJ D-OMMY

DJ D-OMMY kwa mwaka 2017 amepata shavu la kutumbuiza kwenye matamasha ya Rugby After Party yaliyofanyika miji mitatu nchini Marekani.

Mwaka 2017 pia amefanikiwa kutumbuiza kwenye Tamasha la kimataifa la One Africa Music Fest mjini Dubai na katumbuiza pia kwenye matamasha yote ya Fiesta Rwanda na Tanzania.

25-NANDY.

Mwaka 2017, umekuwa ni mwaka mzuri kwa Nandy kwani matunda ya kazi zake nzuri za muziki yameongezeka ambapo ameweza kutwaa tuzo kubwa barani Afrika za AFRIMA.

Nandy

Ni moja ya wasanii ambao kwa mwaka 2017, waliotumbuiza karibia matamasha yote makubwa nchini Tanzania kwa mwaka 2017. Pia amekuwa balozi wa taasisi ya Tulia Trust inayojihusisha na matamasha ya kucheza ngoma za asili.

Kubwa zaidi, Nandy amefanikiwa kurekodi vipindi vya Coke Studio Africa 2017 season 5.

26-MAMI.

Moja ya watangazaji wakike waliofanya vizuri kwenye vipindi vya burudani vya radio, Basi Mtangazaji wa Clouds FM, Mami ni moja ya watangazaji waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka huu.

Mami

Mami amefanikiwa kuwasahaulisha wasikilizaji wa kipindi cha XXL pengo la aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM, DJ Fetty kwa kiasi kikubwa.

Sauti na jinsi ya uuambaji wa maneno akiwa hewani ni moja ya sifa zilizomfanya awe wa kipekee kwa mwaka 2017 na kuwavutia vijana wengi wanaopenda vipindi vya burudani.

Amepata mashavu pia ya matangazo ya bidhaa za Shake & Sippy.

27-HANSCANA.

Hanscana ni mwaka wake wa pili kufanya vizuri kwenye kazi yake ya kuongoza video za wasanii wa muziki wa Bongo Fleva.

Hanscana

Ubora wa kazi zake na kujituma kwake kumewafanya watu wengi wenye lengo la kuja kuwa Ma-director kujifunza zaidi kutoka kwake.

Kwa mwaka 2017, kupitia Kampuni yake ya Hanscana Brand amefanikiwa kushoot zaidi ya video 13 na zote zimefanikiwa kupenya kwenye vituo vya runinga vya kimataifa.

Baadhi ya video alizoshoot ni Turn Up ya Country Boy, Lucky Me ya G Nako, Single ya Abdukiba, Nshalewa ya Nedy, Vitamin U ya Roberto kutoka Zambia na video nyingine kali.

28-FREDRICK BUNDALA (Sky Walker).

Ni moja ya Waandishi wa Habari na Watangazaji wakongwe nchini Tanzania, Kwa mwaka 2017 amefanikiwa kuachia vitabu vitano (Handaki la Kifo, Kimo, Dume Suruali, Simami na Kibuyu cha Ajabu na Mambo 15 yasababishayo Umasikini).

Fredrick Bundala

Ukiachana na Uandishi wa Habari kwa sasa Bundala anafanya kazi na Kampuni ya Afripo kutoka Sweden Kama Meneja Mkazi wa Tanzania.

Mwaka 2017, amefanikiwa kufanya matangazo ya Kampuni ya BIKO na amekuwa Influencer wa Coke Studio Africa.

Kazi ya vitabu vyake unaweza kuipata kwa kupakua App ya Uwaridi na Simu Gazeti ambazo zote zinapatikana kwa watumiaji wa iOS na Android.

29-MR T TOUCH.

Baada ya kutangaza kujitoa kwenye studio za Free Nation zinazomilikiwa na Nay wa Mitego, Mr T Touch mwaka 2017 amefanikiwa kuanzisha Studio yake ya Touchez Sound na kufanikiwa kutoa hit kibao.

Mr T Touch

Bombadier ya Dully Skies, Nishaidie kushare na Bata zote za Jaymoe, Sometimes ya Baraka The Prince, Chovya ya Diana, Kibabe ya Professor Jay, Unaonaje ya Young Killer, Bongo Bahati Mbaya ya Young Dee na ngoma nyingine nyingi ambazo zote zimeshika chati mbalimbali kwenye vituo vya radio na TV ndani na nje ya nchi.

30-DIRECTOR MSAFIRI (KWETU STUDIOS).

Moja kati ya waandaaji wa video ambao wamejitahidi pia kwenye uaandaaji wa video, Msafiri amefanya poa kwa mwaka 2017.

Amejitahidi kuongoza video nyingi kali na ubunifu wake ndio katika kazi ndio umemuweka juu kwa umemfanya awe tofauti kidogo na Madirector wengine.

Wapo watu wengi waliofanya vizuri kwenye Sanaa, Michezo, Ujasiriamali na kwenye Media lakini hawawezi kuwepo wote kwenye orodha lakini mchango wao unatambulika kwenye jamii.

Majina hayo 30 yameingizwa kutokana na maoni ya Wananchi na Vyombo vya Habari tofauti tofauti na kisha kutolewa rasmi mtandao wa Bongo5.com .

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents