Bongo5 Makala

Makala:Soka la Tanzania linashindwa kuendelea kwa kukosa viongozi bora na wazalendo

ABEID PELE (640x425)

Na Yasin Ngitu,

Mchezo wa mpira wa miguu Bongo umekuwa kama ndoto kupata mafanikio. Kadri siku zinavyokwenda, ndivyo tunavyozidi kushuka chini. Ni kweli kuwa Tanzania tunakosa wachezaji? Tunao vijana wengi wenye vipaji.Tangu miaka ya nyuma tumekuwa na makocha tofauti tofauti, wazawa na wageni, hakuna hata mmoja mwenye uwezo wakufundisha mpira?. Lipo tatizo kwenye uongozi ambalo linadumaza mpira wetu.

Kama tupo pamoja mwaka 1965 tulishika nafasi ya 65 katika viwango vya FIFA mpaka sasa tuna miaka zaidi ya 48 hatujawahi kushika nafasi ya juu kama hiyo ukilinganisha na ya sasa ambapo tunashika nafasi 135 kwa viwango vya FIFA na kwa Afrika nafasi ya 41. Tunatoka wapi? Na tunakwenda wapi?

Mafanikio yangekuja kama tungekuwa na viongozi wa soka wabunifu na wazalendo ambao tunawakabidhi taifa lenye vijana wenye vipaji wanaohitaji kuongozwa na mifumo mizuri ya kuwakuza na kuwakomaza ili siku moja na sisi tuonje furaha ya kuchukua kombe kubwa la kimataifa litakalobadilisha mfumo mzima wa mpira Tanzania.

Kiukweli soka la Tanzania limepotea kabisa. Michuano ya AFCON imemalizika hivi karibuni tukiona Burkina Faso inayoshika nafasi ya 92 kwa ubora duniani na mwaka huu ikifanikiwa kufika hatua ya fainali. Kwao hiyo ni hatua kubwa sana katika soka.Lini na sisi tutafikia mafanikio hayo?

Tunaona katika mchakato wa kumpata viongozi watakaliongoza shirikisho la soka nchini, TFF baada ya uongozi uliopo madarakani kumaliza muda wake, kumekuwa na ushindani mkubwa baada ya watanzania kuwa na nia ya dhati ya kutaka kuliinua soka la Tanzania ambapo uchaguzi utakaofanyika February 24.

Ni matumaini yetu tutawapata viongozi watakuwa wenye uwezo stahiki watakaorejesha matumaini ya watanzania waliopoteza matumaini na soka la Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents