Habari

Makamu Rais wa Marekani agoma kula meza moja na dada Rais wa Korea Kaskazini

Makamu rais wa Marekani, Mike Pence amegoma kuwepo katika chakula cha jioni na kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini Kim Yong-nam.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Yo hap Pence alionana kidogo na bwana Kim wakati wakijaribu kukwepana kuonana uso kwa uso.

Wawili hao walikutana katika sherehe za ufumbuzi wa mashindano ya michezo ya Olympiki ya msimu wa baridi. Michezo hiyo inaendelea wakati ambapo kuna mvutano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Bwana Pence na Kim Yong-nam walikuwa wenyeji wa Rais wa Korea Kusini kabla ya sherehe haijaanza huko Pyeongchang, hata hivyo Makamu rais wa Marekani alikaa kwenye tafrija hiyo kwa dakika tano tu na kuondoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents