Afya

Mama ajifungua watoto tisa, aeleza uimara wa afya za watoto wake (+ Video)

Halima Cissé na mumewe Abdelkader Arby wamezungumza kwa mara ya kwanza na RFI tangu kujifungua watoto wake tisa mwezi Mei. Bi Cissé alibainisha kuwa mmoja wa watoto wake wa kiume wamempa jina la Mohammed VI kwa heshima ya mfalme wa Morocco, kutokana nay eye kujifungua Casablanca ambako watoto wake wameendelea kuwa chini ya uangalizi katika mashine ya kukuzia watoto.

‘’Nimekumbuka nyumbani,binti yangu mkubwa, familia yangu na marafiki zangu, ‘’Bi Cissé aliiambia idhaa ya RFI akiwa hospitalini. ‘’Lakini ni suala la muda tu pale tutakaporejea kwa kutegemea hali ya afya ya watoto .’’

Daktari wake Khalid Mseif ameeleza namna mama huyu watoto tisa alivyo shujaa na mtulivu, ameiambia RFI kuwa watoto ‘’ wako vyema’’ baada ya kupona kutokana na athari za kuzaliwa mapema kabla ya muda wao’’.

Kwa sasa wanaelezwa kuwa wanaweza kunyonya maziwa wenyewe na hawatumii tena dawa.

Mdogo kuliko wote, Hawa, bado anahitaji oksijeni na uangalizi wa karibu wakati wa kunyonya.

‘’Tunafahamu kuwa suala hili liko njeya uwezo wetu’’. Bw. Arby alieleza kuhusu shauku kubwa ya vyombo vya habari tangu kuzaliwa kwa watoto miezi mitatu iliyopita. ‘’Ninapenda kumshukuru kila mmoja aliyetusaidia na anayeendelea kutusaidia.’’

Bofya hapa chini kuwasikiliza.

https://www.instagram.com/tv/CSHKuyrDnaE/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents